Dkt.Migiro, amshukuru Rais, aipongeza Wizara kwenye michezo



Na John Mapepele, London

Balozi wa Tanzania, nchini Uingereza. Dkt, Asha Rose Migiro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa jicho la pekee kwenye sekta ya  michezo.

Mhe Balozi Migiro ametoa kauli hiyo leo Julai 29, 2022  nchini Uingereza kwenye mashindano ya Michezo ya  Jumuiya ya Madola ambapo Tanzania inashiriki.


"Hapa napenda kusema  kwa dhati kama Balozi mwanamke wa Tanzania hapa Uingereza kuwa  namshukuru Mhe. Rais kwa kutoa kipaombele kwenye michezo na sasa tunaona mafanikio makubwa kwenye michezo ya wanawake' ameongeza Mhe. Migiro


Hadi sasa tayari timu ya taifa ya soka ya wanawake  chini ya umri wa miaka 17 ( Serengeti Girls) na timu ya taifa ya wanawake ya  Kabbadi zimefuzu kuingia kwenye  mashindano ya dunia ya michezo  hiyo.

Aidha, amempongeza wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kazi nzuri inayofanya ya kuitangaza  Tanzania duniani kupitia michezo.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa mwaminifu kwenye  Jumuiya.

"Tunaishukuru pia wizara  tumekuwa na ushirikiano na  umechangia umadhubuti wa mashindano" amefafanua Mhe. Migiro



Pia amesema ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Michezo wa nchi za Jumuiya  za madola umekuwa na umuhimu kwa  vile ndiyo mkutano unaotengeneza Sera na mipango mbalimbali. 

Katika mkutano huo mambo kadhaa yamejadiliwa ikiwa ni pamoja na   haki za binadamu na  umuhimu wa kuheshim na kulinda utu wa wanamichezo 

Pia mbinu mbalimbali za kuwekeza kwenye   michezo.
Previous Post Next Post