Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amesema serikali inapopandisha mishahara inaangalia zaidi kima cha chini na kwamba asilimia 23 iliyosemwa na Rais Samia Suluhu siku ya Mei Mosi iliwalenga zaidi wenye kipato cha chini.
“Asilimia 23 iliyotamkwa haijalipwa kwa watumishi wote, fomula iliyotamkwa si wote mpaka wenye mishahara mikubwa, walionufaika ni wenye mishahara midogo.-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ufafanuzi nyongeza ya mishahara.”
“Hao wanaosema tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye asilimia 22, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha” Mhe. Majaliwa, akifafanua nyongeza ya mishahara.