SHIRIKA LA WAYDS WANG'ARA MKUTANO WA AFYA TANZANIA





Shirika la WAYDS limeandaa mkutano wa Afya Tanzania (TANZANIA MENTAL HEALTH SUMIT 2025) uliofanyika Kahama mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Hospital ya Taifa ya Miembe, Foundation Botnar, Vitol Foundation, Doctor with Africa(CUAMM).


Mkutano huo ambao wenye kaulimbiu isemayo “HATUA SHIRIKISHI NA JUMUISHI: KUKUZA USHIRIKIANO KATIKA AFYA YA AKILI KWA MAENDELEO ENDELEVU”, uli kuwakutanisha wadau mbali mbali kwa ajili ya kujadili ajenda kuuu ya afya ya akili kwa Tanzania, kuandaa jukwaa la pamoja la kuhamasisha wadau na watunga sera pamoja na jamii kwa ujumla kushughulikia changamoto za afya ya akili kwa kuandaa mikakati ya utekelezaji kwa ajili ya kuboresha huduma na ustawi wa afya ya akili katika jamii zetu.

Mkutano utakuwa unafanyika kila mwaka kuazia mwaka 2025 na Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama,

Shughuli zilizofanyika katika mkutano huo pamoja na mawasilisho kutoka kwa wataalamu wa afya ya akili, mijadala na mafunzo kwa vijana juu ya uelimishaji wa afya ya akili katika jamii, warsha mbalimbali na maonesho ya afua mbalimbali zinazotekelezwa na wadau wa afya ya akili ndani na nje ya Tanzania.




Mkutano ulifanyika kwa siku mbili kuazia ke tarehe 30 na 31 mwezi huu wa tano 2025 na ulihudhuriwana wadau zaidi ya 300 wadau wa nje Nchi ambao ni Foundation Botnar, Embassy of Sweden, WHO, UNFPA, Doctors with Afrika, Science for Africa Foundation, Africa Academy for Public Health, Grand Challenges Canada, United for Global Mental Health, Save the Children International. Wadau wa ndani ambao ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hospitali ya Taifa ya afya ya akili, Tanzania Health Medical Education Foundation, Tanzania Psycchological Association, na vijana mbali mbali kutoka kila Mkoa wa Tanzania.

Shirika la WAYDS limetoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla kuwekeza katika Afya ya akili ili kujenga Taifa letu kiuchumi.





Previous Post Next Post