WAZIRI UMMY: HAKUNA MGONJWA MPYA WA HOMA YA MGUNDA YA



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwa mujibu wa ufuatiliaji wa wataalam walioko mkoani Lindi juu ya ugonjwa wa homa ya Mgunda uliotolewa taarifa Julai 18 mwaka huu, inaonesha kuwa toka tarehe 18 Julai 2022 hadi sasa hakujawa na mgonjwa mpya aliyeonesha dalili za ugonjwa huo. Hivyo hadi kufikia asubuhi ya leo Julai 29, 2022, idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuugua ugonjwa huo nchini ni 20 na na kati yao 3 wamefariki.

Waziri Ummy amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya ugonjwa huo, ambapo amesema wagonjwa wote wameruhusiwa kurudi nyumbani na wanaendelea na vizuri na kuwa ugonjwa huo unatibika kwa kutumia dawa ambazo zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini. Aidha, timu ya ufuatiliaji imebaini kuwa, miongoni mwa watu waliotangamana na wagonjwa hao hakuna aliyeonyesha dalili za ugonjwa huo hadi kufikia sasa.

"Hii inadhihirisha pia, ni mara chache ugonjwa huu huambikizwa kutoka binadamu mmoja
kwenda kwa mwingine. Vilevile, wataalamu wetu wanaendelea na utafiti wa kina kwa binadamu, wanyama na mazingira yanayowazunguka ili kubaini na kuweka mikakati ya kuudhibiti ugonjwa huu nchini.

Ndugu wananchi, Maandiko ya kisayansi yanaeleza kuwa, kwa kawaida ugonjwa huu unakuwa na dalili ambazo sio kali kwa asilimia 90, isipokuwa kwa wagonjwa wachache, (asilimia 10), wanaweza kuwa na dalili kali kama kutokwa na damu na kuathirika kwa viungo kama figo na Ini," amesema Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya 

Previous Post Next Post