WAZIRI JAFO AAGIZA UFUMBUZI WA CHANGAMOTO ZA KISHERIA ZINAZOATHIRI USHINDANI KWA WAFANYABIASHARA.





Na Lilian Ekonga..........

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe, Selemani Jafo amemuelekezea katibu Mkuu wizara ya hiyo kuwasilisha changamoto zote za kisheria na w kanuni zinazo kwamisha wafanyabiashara kushidwa kushiriki vizuri katika upande wa ushindani na zitafutiwe ufumbuzi ili kuhakikisha sekta ya biashara inakuwa nchini.


Waziri Jafo ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani Duani ambapo amesema
serikali ya awamu ya sita inaboresha miundo mbinu ili kuhakikisha sekta ya Biashara inakuwa kwa kasi m kuongeza ushindani halili wa bidhaa katika masoko ya kitaifa.




Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameagiza mijadala yote itakayojadiliwa katika maadhimisho hayo iwasilishwe kwake ndani ya siku kumi na nne ili kufanyia kazi mawazo yaliyojadiliwa kwa lengo la kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara na ushindani wa bidhaa.


Alikalika waziri amemuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Fcc kuimarisha mifumo ya kibiashara ikiwemo michakato yote ya maunganiko ya kampuni wanaifanye kwa haraka ili vijana wa kitanzania waweze kupata ajira hasa wanaomaliza vyuo vikuu.

"Yale makampuni yanayotaka kuongeza ushalizaji hasa katika miunganiko ya kamapuni hayo, endeleni kwa haraka lengo kubwa ni kwamba tuweze kuhakikisha uwekezaji tunauchagisha"amesema

Pia Amesema Mkutanao huo utawezea kuleta fursa mbalimbali za uwela wa mambo mbalimbali ya kisheria na kikanuni yanohusu maswala ya ushidani.

Aidha waziri amewataka vijana wakitanzania kwa wale watakao pata fursa ya kupata ajira katika maeneo mbalimbali, kuhakisha wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa katika upande wa viwanda na sekta binafsi.




"Watumishi wa serikali hakikisheni kwa yale mnayoona mnaweza kusaidia ili uwekezaji uende kwa haraka na makampuni hakikisheni mzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji na kutokufanya udanganyifu wowote." amesema jafo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa tume ya FCC Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa tume hiyo inawajibu na kusimamia uwepo wa fursa sawa kwa washindani wakubwa na wadogo katika soko, na kupunguza ukiritimba katika masoko kwa kuhakikisha washindani wakubwa hawawazuii washindani wadogo kukua na kuingia au kuwatoa sokoni.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Wiliam Erio amesema hayo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya ushindani duniani tangu kufanyika marekebisho ya sheria nchini.




"Tunamshukuru sana Rais samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge kwa kufanikisha kupitisha kwa marekebisho na kuwa sheria jambo ambalo litatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

kila ifikapo December 5 kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya ushindani Duniani ambapi Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es salaam na kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni "Sera ya ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi"
Previous Post Next Post