TFRA YAWAHIMIZA WAKULIMA KUJISAJILI


Na Humphrey Msechu,Dodoma

Kaimu Mkurugenzi  wa Uzalishaji wa Ndani na Ununuzi wa Mbolea kwa pamoja, Bw. Louis Kasera amewaasa wakulima kujisajili mapema ili wapate mbolea ya ruzuku itakayowawezesha kuzalisha mazao kwa tija.

Akizungumza na waandishi wa habari kwwnye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) amesema malengo ya setikali ni kuandikisha wakulima milioni saba lakini mpaka sasa waliojisajili ni wakulima milioni nne tu.

Hata hivyo amesema hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka msimu wa kilimo ujao wawe wamefikia idadi iliyotarajiwa.

Aidha amesema kwa ambao walishajisajili kipindi cha nyuma wanapaswa kuuhisha taarifa zao kwa alama za vidole ili mkulima ajulikane alipo lakini pia ijue mkulima huyo ni nani.

"Ninachoomba wakati wa kujisajili na kuuhisha taarifa zao,watoe taarifa sahihi ili waweze kufikiwa walipo."amesema Kasera

Vile vile  amesema mbolea ipo ya kutosha hivyo amewaasa wakulima wanunue mbolea mapema ili kuangalia kwenye mapungufu ipelekwe huko.

"Kwa sasa msimu ndiyo umeanza lakini tuna tani 300,000 za mbolea ya kupandia na kukuzia ."amesema Kasera

Kwa mujibu wa Kasera,hali ya mbolea ni ya kutosheleza huku akisema mwaka huu lengo ni kufikia tani milioni moja na kwamba asilimia 30 tayari ipo ndani ya nchi na bado kuna meli zipo njiani zimebeba mbolea .

"Hadi Disemba zote zitakuwa zimesgaingia,na hizo ni zile zinazotoka nje ,bado zinazozalishwa katika viwanda vyetu vya ndani."amesema 

Kasera amesema ,hapa nchini kuna viwanda viwili cha Minjingu na Intracom ambavyo vina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 850,000.

"Matarajio ya kiwanda cha Itracom ni kuzalisha tani zaidi ya laki sita,na Minjingu tani zaisi ya 250,000 ,kqa hiyo utaona viwanda vya ndani uzalishaji wake ni zaidi ya asilimia 50 ,lengo la serikali ni kuondoa utegemezi ,tunataka ifikapo 2030 tuwe tunajitosheleza kwa mbolea ya ndani."amesisitiza
Previous Post Next Post