RC SENYAMULE AKABIDHI WAKUKULIMA ZAIDI YA MAREKTA 10 KUTOKA PASS LEASING



Na Humphrey Msechu, Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule aipongeza kampuni ya PASS LEASING kwa kuweza kuwazamini wakulima mikopo ya vifaa  vya kilimo kwa lengo kufanya shuguli za kilimo kwa kutumia teknolojia ya kisasa badala ya kutumia nguvu na mikono haya ni mapinduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo .

Senyamule ameyasema hayaoa wakati  akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya  wakulima mifugo na uvuvi  Nane nane jiji Dodoma ambapo amesema ile kauli ya kusema kilimo ni uti wa mgongo isiwe kwa maneno bali iwe kwa vitendo  na tunaona sasa wakulima wanaendelea kuelewa umuhimu wa kutumia vifaa vya kisasa
Na wakiendelea kuamini juhudi kubwa zinazofanywa na serikali  ya awamu ya sita

Amesema wanaendelea kuona wadau mbalimbali wakiunga mkono juhudi zinazofanyika katika sekta ya kilimo 


 Amesema  wamegawa matrekta 12,Gari moja la kubebea mizigo,mashine ndogo ya kuchakata mazao, yote haya yanaenda kuleta mabadiliko  makubwa kwa watumiaji wa zana za kilimo waliokuwa wanalima kwa mkono  sasa wanaanza kulima kwa kutumia Trekta na kama mnavyojua kilimo cha kutumia zana za kilimo kama Trekta.

Amesema tunajua faida", ya kulima kwa kutumia trekta kwasababu watalima heka nyingi kwa wakati mmoja na  hawa wakulima hawatalima mashamba yao tu bali watalima na mashamba ya wengine katika maeneo yao maana yake kwa kukodisha wengine
Amesema Senyamule.

Nawapongeza sana kampuni ya PASS LEASING kwa utashi huu mkubwa milio nao na mmezamilia kusaidia kundi hili la wakulima ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania niwapongeze sana kwasababu serikali inaanzisha mpango lakini inafanya kazi na wadau mbalimbali ili kufikia malengo yake.

Amesema kuwa hayo wanayoyafanya ni wazi kwamba wamemulewa vizuri Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan na nimeona mmeshiriki vyema kwenye maonesho haya ya wakulima maarufu nane nane kwa kuyapa thamani Fahari na yakuongezea hadhi

Ameongeza kuwa wakulima waliopata hivyo vifaa waende kuvitumia kwa uangalifu mkubwa kwa umakini mkubwa kwani kufanya hivyo itakuwa faida kwa wengine na hapa waliopata wametoka mikoa tofauti ikiwemo Dodom, Morogoro,singida  na Manyara na tunategemea mwaka kesho mje na shuhuda.

Amesema mpango huu unawalahisishia wakulima kupata vifa bila kuwa fedha taslimu halafu watalipa deni ndipo upate hati kwani Mapango huu ni mzuri unawarahishia hata wale wasio kuwa na uwezo wa kifedha.

Na kwa upande wake Mnafaika Minza Mlela  ameishukuru kampuni ya PASS LEASING kwa kumkubadhi Trekta ambayo itaenda kufanya Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo na nakumlahisishia katika shughuli zake za kilimo 

Hapo awali alikuwa analima heka 200 kwa kutumia mda mrefu saa hivi ataweza kulima kwa mda mfupi pia ataweza kukodisha wakulima wenzake kwani na wao watanufaika.

Kwa upande wake Mnafaika mwingine Awichi Njarika mkazi wa Pandambili wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma amesema uko nyuma alikuwa analima kwa  kutumia jembe la mkono  badae akapata matarekta ila kwasa ameishukuru PASS LEASING kwa kuweza kuwakopesha Trekta mpya 

Amesema wakulima wenzake waachane na Mtarekta ya zamani kwasababu kuna fursa za mikopo waende waongee na makampuni pamoja na taasisi za kifedha  ili wanunue Trekta nzuri ili waweze kusogea mbele kiuchumi.


Previous Post Next Post