INEC YABORESHA MFUMO WA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Tume Huru ya  taifa ya uchaguzi(INEC), imesema  imeboresha mfumo wa uandikishaji ambao kwa mara ya kwanza ya kwanza utamuwezesha mpiga kura aliyekuwepo kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura nchini kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake

Pia mpiga kura anaweza  kuhama kituo kwa kutumia simu au kompyuta  na baadae  kutembelea kituo anachokusudia  kujiandikisha ili apatiwe kadi yake ya mpiga kura.


Hayo yamesemwa leo juni 13, 2024 na Mwenyekiti qa Tume Huru ya  Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano 
Kati ya Tume na waandishi wa vyombo  mbalimbali vya  habari nchini.

Amesema wakati wa zoezi hilo tume imeweka  utaratibukwa watu wenye ulemavu, wazee, wagojwa wajawazito n wakina mama wenye watoto wachanga watakao kwenda nao vituoni kupewa fursa ya kuhudumiwa bila kupanga foleni.

"Tunawaomba waandishi wa habari kupitia kalamu zenu muwafahamishe wananchu wote waliopo kwenye makundi tajwa kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha au kuboresha taarifa zao vituoni kwa utaratibu mzuri"amesem jaji Mwambegele.


Ameongea kuwa  uboreshaji huo  unatarajiwa kuzinduliwa rasmi julai Mosi, 2024 mkoani kigoma n  Waziri Mkuu  wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Amesema wananchi wanapaswa kupata taarifa sahihi kuhusu kujiandikisha na umuhimu wake, hivyo Tume imejikita katika kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa ili uboreshaji uwe wa mafanikio.

Ameeleza kuwa Mifumo miwili itatumika ukiwemo wa (VRS) Mfumo Mkuu na (OVRS) ikiwa ni mfumo kwa njia ya mtandao.

Amesema mifumo yote miwili itahusisha fomu tatu, Namba moja, Kuandikisha wapiga kura wapya, Namba 5A wanaoboresha taarifa zao, wanaohama vituo, waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika, na namba 5B kuondoa taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za kuwepo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.


Uandikishaji wa wapiga kura utahusisha uchukuaji wa alama za vidole vya mikono, picha na saini na kuhifadhiwa kwenye kanzidata ya wapiga kura.

Ameongeza kuwa uboreshaji wa Daftari wa mwaka 2024/2025 utatumia teknolojia ya BVR Kits zilizoboreshwa kwa kuwekewa program endeshi ya kisasa zaidi.
Previous Post Next Post