WAKUNGA NCHINI WAMETAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU STAHIKI KATIKA JAMII ILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Wakunga nchini wametakiwa kuendelea kutoa elimu stahiki katika jamii itakayowezesha kuendelea kupunguza na kuokoa vifo vya mama na mtoto, ili kuchangia katika mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu kwa kupunguza vifo vya watoto na kuboresha afya ya uzazi.

Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais wa chama cha wakunga Tanzania Loveluck Mwasha wakati wa mdahalo uliowajumuisha wadau mbalimbali, ikiwemo shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA, wadau wa afya kutoka sekta mbalimbali, na viongozi vya serikali wenye lengo la kujadili namna sahihi ya kuendelea kuokoa maisha ambapo amesema vifo vingi vya mama na mtoto vinachangiwa na kuzaa katika umri mdogo. 

"Tumekutana hapa kuweza kuangalia ni zipi changamoto na nini tufanye kama wadau ili kuondoa hizi chagamoto na kupunguza vifo vya mama na mtoto"amesema Mwasha

Kwa upande wake Meneja wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka UNFPA Felister Bwana, amebainisha kuwa wakunga wanayo nafasi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa asilimia 64, huku akieleza changamoto pekee inayoikabili sekta ya ukunga nchini ni idadi ndogo ya wakunga nchini, pamoja na elimu duni. 

Ameongeza kuwa pamoja na juhudi ambazo zinafanywa na serikali na wadau bado tatizo lipo na juhudi za makusudi zinatakiwa hasa kuboresha hali ya wakunga

"Asilimia ubwa ya wanawake wanakufa kwa kwasabab ya kutoka damu baada ya kujifungua na kifafa cha uzazi karibia asilimia 50"amesema Felister. 

Kila ifikapo tarehe 5 mwezi wa 5 kila mwaka, dunia inaadhimisha siku ya wakunga yenye lengo la kutambua, kuthamini na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Wekeza katika Elimu ya ukunga, kupata wakunga mahiri.
Previous Post Next Post