RAIS SAMIA AMERIDHIA KUONGEZA MUDA WA MANUNUZI KWA WAKAZI WA MAGOMENI KOTA


Na Lilian Ekonga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwaongezea muda wa manunuzi, wakaazi wa Magomeni Kota kutoka miaka kumi na tano (15) iliyoelekezwa na Serikali awali hadi kuwa miaka thelathini (30) ikijumuisha miaka mitano (5) ya kukaa bure.

Gharama za awali za ununuzi wa nyumba hizo ni Milioni 48,522,913.00 kwa nyumba ya chumba kimoja na Milioni 56,893,455.00 kwa nyumba ya vyumba viwili kwa muda wa miaka 15 ya ununuzi ikijumuisha miaka 5 ya kukaa bure.


Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amsema baada ya waakazi wa Magomeni Kota kujulishwa juu ya gharama hizo, wakaazi walimuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwapunguzia gharama za ununuzi wa nyumba hizo pamoja na kuwaongezea muda wa kulipia.

"Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua nyumba za Magomeni Kota mnamo Machi 23, 2022
alitoa maelekezo ya wakaazi wa Magomeni Kota kuuziwa nyumba hizo kama Wakaazi
Wanunuzi bila kuzingatia gharama za thamani ya ardhi, maeneo jumuishi kama ngazi na lift pamoja na mandhari ya nje."


"Baada ya timu ya wataalam kufanya tathmini kwa kuzingatia maelekezo ya Rais ilikuja na gharama za ununuzi wa nyumba hizo ambazo ni Milioni 48,522,913.00 kwa nyumba ya chumba kimoja na Milioni 56,893,455.00 kwa nyumba ya vyumba viwili kwa muda wa miaka 15 ya ununuzi ikijumuisha miaka 5 ya kukaa bure."

Kutokana na hivyo Kondoro alizitaja gharama na utaratibu mpya wa mauzo ya nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es Salaam 

"Nyumba ya chumba kimoja inauzwa Shilingi 48,522,913.00 na muda wa malipo ni miaka 30."


"Nyumba ya vyumba viwili inauzwa Shilingi 56,893,455.00 na muda wa malipo ni miaka 30." Amesema Kondoro

Aidha Arch. Kondoro amesema Baada ya kuwajulisha kwa barua wakaazi 644, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iko tayari kuwatambua wakaazi waliotayari kutekeleza utaratibu huu wa
ulipaji na kuingia nao mkataba wa mkaazi mnunuzi.

Pia Arch. Kondoro amesema Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iko tayari kuwatambua wakaazi wasiokuwa tayari kutekeleza utaratibu huo ambao wataruhusiwa kukaa bure kwa miaka mitano (5) na baada ya muda huo kukamilika, nyumba watazirejesha Wakala wa Majengo Tanzania (TBA
Previous Post Next Post