TUCTA YAIOMBA SERIKALI KUTAZAMA UPYA VIWANGO VYA KODI NA MISHAHARA


Na Mwandishi wetu. 

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tucta limeiomba serikali kutazama kwa upya viwango vya kodi na Mishahara katika sekta ya umma na binafsi ili kuweza kuboresha Masilahi kwa Mfanyakazi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mapema leo Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) Said Wamba amesema kuwa nivyema serikali ikaboresha Viwango vyakodi kwa wafanyakazi wa umma sambamba na Mikataba ilikuboresha halibora kwa Mfanyakazi wa Umma.

"Tunaiomba Serikali ifanyie Marekebisho ya Bima ya Afya ilikuweza kumnufaisha Mfanyakazi kwasektavyaumma bila kuumia"amesema Said Wamba

Naibu Katibu Mkuu ameongeza kuwa nivyema serikali kujenga utamaduni wa kutana na vyama vya wafanyakazi ili kuweza kujadili Mara kwa Mara changamoto za wafanyakazi nakuzitafutia ufumbuzi.

Aidha amesema Nivyema wafanyakazi katika sekta yaumma kuendelea kufanyakazi kwa ufanisi zaidi na tija ilikuweza kuishawishi serikali kufanya Marekebisho hayo ya Mishahara na kodi.

"Wito kwa wafanyakazi wote nchini kuongeza tija katika kazi ilikuweza kupata Nguvu ya kudai Nyongeza ya Mishahara "Aliongeza Said Wamba. 

Wamba alisisitiza kuwa Nivyema Watumishi wa uuma kuzingatia Muda wa wakazi uendane sambamba na jasho Lao.
Previous Post Next Post