ZAIDI YA VIJANA 10OO WATUMA WAOMBI YA UFADHILI WA MAHARI KWA TAASISI YA ALKHIMA FOUNDATION


Na Lilian Ekonga

Mwenyekiti wa Taasi ya Alkhima Foundation  Sheikhe Nurdin Kishki ametoa rai kwa watanzania kukubali kuoa ama kuolewa ili kuepukana na mmongonyoko wa maadili hususani ndo za jinsia moja amabazo zinaletwa na tamaduni za mataifa ya nje ya nchi.

Kauli hiyo ameitoa leo aprili 9 jijini dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na nia ya kuwalipia mahari vijana 50 ambapo wapo tayari kuoa kama sehemu ya programu yao ya kuleta manufaa katika jamii kupitia mashindano yakusoma Quran yalifanyika hivi karibuni

Amesema kuwa zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya nchi wametuma maombi ya kuhitaji ufadhili huo hata kabla ya utaratibu rasmi kutangazwa.

Kishki amesema wamezindaa fomu ambazo mwanzo wa kuchukua itakuwa kuanzia leo tarehe 13 mwezi wa nne na mwisho wa rudisha foma ni tarehe 2 ya mwezi wa tano na wameweka wiki mbili na fomu zitapatikana alkhima foundation makao makuu temeka jijin dar es salaam. 

"Tunatamani kuwatoa vijana kimaisha na tunatamani kutoa hata misingi lakin mambohuanza polepole ila kwa sasa tumeamua kuanza kuwatoa wanaohitaji kuoa ambapo wanauwezo wa kupata ridhiki ila kinachowashinda ni mali ya mkupoa ndo tutakao wasaidia " amesema shekhe Kishki. 

Ameongeza kuwa number za kuweza kuwasilia na wanakamati kwaajili ya kupokea watu mbalimbali wanaohitaji hilo swala na kuwapa fomu 0789 407045 au 0658 423444.

Hata hivyo amendelea kuwaasa watanzania na umma waendelee kuwaunga mkono kama mashirika mbalimbali pamoja na mabenki katika kuhakikisha jambo hilo lifanikiwa na endapo watapata watu zaidi wa kuwaunga mkono hata idadi ya watakolipiwa mahali inaweza ikaongezeka zaidi.

"Vijana hao hatutawakabithi majiko mpka tuwape semina mahalumu ya kuweza kukaa na wake zao na tutafuta wakufunzi maalimu kwaajili ya masomo ya ndoa vijana tutawafunza kwa siku moja nzima tutawafundisha dhamani ya ndoa na namna ya kufuvuliana" amesema. Shekhe Kishki.

Aidha amesema sasa hivi kumekuwa na wimbi la kwenda kinyume na Mungu ambapo ulimwengu wa kizungu umekuja kutubadilisha kuwa na ndoa ya jinsia moja watanzania tuna Mungu wenzetu hawana dini wala Mungu hata huu mtindo wa kuozesha vijana ni moja ya mtindo wa kuepusha mmongonyoko wa maadili.
Previous Post Next Post