Benki ya maendeleo PLC imevunja rekodi kwa mwaka 2022 kwa kuwa benki yenye faida kwa miaka 8 mfululizo ambapo faida kabla ya kodi ikiwa ni bilioni za kitanzania 1.984 ukuaji wa mwaka wa 181% na faida baada ya kodi ikiwa ni bilioni 1.415 ukuaji wa mwaka wa 141%.
Hayo ameyasema Mkuu wa kitengo cha Biashara wa maendeleo Benki, Emmanuel Mwaya wakati akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam ambapo amesema kupitia mafanikio hayo, wataendelea muongeza mahusiano ya wateja, ari ya utendaji ya wafanyakazi itaongezeka,
"Baadhi ya vichochezi vya faida hiyo ni ukuaji wa jumla wa mapato kwa asilimia 26 mwaka hadi mwaka kutoka bilioni 14.23 hadi bilioni 17.97 kwa mwaka 2022, Mapato ya riba yalikua kwa asilimia 31 kutoka bilioni 7.6 mwaka 2021 hadi bilioni 9.9 mwaka 2022"
Aidha ameongeza kuwa jumla ya mapato ni shilingi Bilioni 12 ikiwa ni ukuaji wa mwaka wa 31%, ambapo uwiano wa gharama kwa mapato ni 58% , jumla ya mali ni bilioni 107.1 ikiwa ni ukuaji wa mwaka 5%, amana bilioni 72.0 ikiwa ni ukuaji wa 11% lakini pia mikopo bilioni 61.0 ikiwa ni ukuaji wa 5%.
Amesema vichochezi vingine ni biashara ya mikopo iliyotokana na uimarikaji wa hali ya uchumi, usimamizi wa karibu wa mikopo iliyotolewa na usimamizi thabiti wa mahusiano yao mazuri na wateja .
Hata hivyo Mwaya amesema Benki imeendelea kuonyesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi huku uwiano wa gharama za mapato ukiongezeka hadi 58% kutoka 74% katika kipindi kama hicho mwaka jana ukiwa na nia ya kufikia kiwango elekezi kutoka bilioni 57.7 hadi bilioni 60.6 Mwaka 2022
Kuhusu Amana, Mwaya amesema mbinu iliyotumika katika uhamasishaji na ukuaji wa amana kwa wateja, ulichagiwa kwa kiasi kikubwa uboreshaji wa huduma na bidhaa bunifu ambazo benki imekua ikitoa.
"Kuongezeka kwa bidhaa za kidigitali kama vile huduma za kibenki kwa simu, huduma za uwakala ambapo zaidi ya benki mawakala 1,300 zimechangia ukuaji huu unaoshuhudiwa leo hii"
Kuhusu Jumla ya mali, Mwaya amesema benki iliimarika kutoka bilioni 102 hadi bilionu 107 ikiwa ni ukuaji wa 5%.
Benki ya maendeleo inaendelea kuwekeza kwenye teknolojia kwa kutambulisha bidhaa za kidijitali kama Internet banking, mfumo wa ukusanyaji wa malipo , mkopo kwa njia ya simu n.k ambapo itawezesha benki kupata mizania ya mtaji zaidi ya 10% kwa mwaka 2023 na kuboresha njia mbadala kwa wateja wao.