RAIS MSTAAFU JOAQUIM AMETOA WITO KWA KAMISHENI YA KISWAHILI AFRIKA KUENDELEZA MATUMIZI YA KISWAHILI


Na Mwandishi Wetu, Dar es salaaam

Wito umetolewa kwa kamisheni ya kiswahili ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Mbaraza ya kiswahili ya nchi na wanachama kuendeleza matumizi ya kiswahili katika maeneo muhimu ya kiutawala na kijamii kwani kiswahili ni tunu na utambulisho wa afrika na mwafrika

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam Aprili 13 na Mhe. Joaquim Chissano Rais mstaafu wa Msumbiji wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Taifa ya Mwl. Nyerere ya Uandishi Bunifu ambapo amesema kiswahili ni tunu na utambulisho wa afrika na mwafrika

Akiongelea kuhusu tuzo hizo Mhe. Chissano amesema Juhudi za kutambua mchango wa wadau wa maandiko bunifu kwa lugha ya kiswahili ni muhimu na kwamba juhudi hizi ziendelezwe kwani uhai wa lugha yoyote duniani ni kuwapo na machapisho yaliyoandikwa kwa lugha hiyo


"Ni wazi Mwl. Nyerere kwa dhati kabisa aliikuza lugha ya kiswahili kwa kuandika maandiko bunifu kama riwaya, mashairi na kutafsiri kazi mbalimbali za fasihi ya kingereza katika kiswahili hivyo ni heshima kubwa tuzo hii kupewa jina lake,"amesema Mhe Chissano  

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Wizara imejipanga kuhakikisha utoaji tuzo za uandishi bunifu unakuwa endelevu na kwamba itahusisha nyanja mbalimbali ikiwemo uandishi wa vitabu vya watoto ili kujenga tabia ya watoto kujisomea wakiwa wadogo na zitakuwa zikitolewa kila mwaka Aprili 13.


Amesema lengo la tuzo hizo ni kuwatambua na kuwazawadia waandishi bunifu mahiri katika nyanja mbalimbali, kukuza lugha ya taifa ya Kiswahili, vipaji vya uandishi bunifu kwa Watanzania, kuongeza hamasa ya Watanzania kujisomea, kuhifadhi historia, amali na kukuza sekta ya uchapishaji na hifadhi za vitabu kwa shule, vyuo na maktaba zetu.  

Nae Waziri wa Elimu Mhe Adolf Mkenda ameipongeza Taasisi ya Elimu (TET) kwa kuhakiksha tunapata vitabu vya kusoma na kulibeba hilo ukumu kwa juhudi kubwa, pia amewashukuru washiriki wote waliotoka mbali kuja kushiriki tuzo hizi. 


Baadhi ya washindi walioshinda tuzo hizo ni pamoja na Dickson Damas Mtalaze kutoka Dar es salaam ambae amekuwa mshindi wa pili katika uandishi wa Riwaya inaitwa Kigodoro Kimeniponza.
Previous Post Next Post