Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba Akizungumza katika tukio hilo la ukabidhaji wa vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 na uzinduzi wa Maabaraya TEHAMA.
NA MWANDISHI WETU
DAR ES SALAAM.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imeunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta ya Elimu kwa kuchangia vifaa vya tehama kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Kimbiji ya Dar es Salaam sambamba na kukabidhi vifaa vya Kielektroniki kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022)kutoka nchini Korea.
Katika tukio hilo, lilienda sambamba na ugawaji wa vyeti kwa Walimu 20 waliopata mafunzo ya tehama kwa kupata Vishikwambi pamoja uzinduzi wa Maabara ya tehama shuleni hapo kupitia mradi huo wa KLIC 2022.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba amemshukuru Serikali kuwekw juhudi sekta ya elimu na mahusiano bora ya Kimataifa na Korea.
"Naomba nimshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, tunafahamu kwamba kupitia Wizara ya Elimu, walimu wote wamepata vishikwambi, na nina imani walimu hapa mnavyo vishikwambi,
kwa hiyo TET tumechangia kwenye juhudi za Rais wetu kwa kuongeza vishikwambi hivyo kwa lengo la kuhakikisha sasa kweli tunaenda kidijitali." Amesema Dk Aneth Komba.
Aidha, amewataka walimu hao kufundisha na kuongeza teknolojia katika manufaa bora ikiwemo kuwawezesha wanafunzi kupata fursa ya kutumia vifaa hivyo vya mradi wa KLIC 2022.
"Tufundishe kwa njia zile za zamani za kitamaduni, lakini pia tukunbuke kuboresha ufundishaji wetu kwa njia bora ya kutumia vfaa vya tehama.
"Vifaa hivi vitasaidia utafutaji wa maarifa, watoto watumie vifaa hivi kuongeza maarifa yao, lakini pia TET inaomba kuhakikisha vinalindwa." Amesema Dk. Aneth Komba.
Aidha, amebainisha kuwa, Kwenye mitahala mipya elimu ya teknolojia imesisitizwa zaidi kwani inaandaliwa na itakapokuja itasaidia wanafunzi na watakuwa bora zaidi.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari kimbiji, Joseph Kiseke ameshukuru kwa uzinduliwaji wa maabara hiyo ya TEHAMA na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.
Kwa upande wao baadhi ya walimu waliopatiwa vifaa hivyo vya tehama wamesema vitakuwa msaada kwao kwani vitawarahisishia katika kufundisha wanafunzi kwa urahisi.
Vifaa vilivyokabihiwa ni pamoja na 'UPS 26, computure Monitor 25, system Unit 25,Wirless keyboard 35, projector moja, scanner moja, printer moja, wireless mouse 35, headphone 25, electric blackboard moja, webcamera 26, digital podium moja, wired keyboard 25,wired mouse 25, speaker 26, adapter 49 na usb flash disk 50'.
KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa Walimu 20 shule ya sekondari kimbiji.