WAZIRI GWAJIMA: KAMPENI YA TWENDE PAMOJA KUZINDULIWA APRIL 27, 2023


Na lilian Ekonga

Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima ametangaza uzundizi wa kamapeni ya Twende pamoja ambayo itatangaza fursa za kiuchumi sambamba na kukataa ukatili wa kinjisia kwa watoto.

Hayo ameyasema leo jijini dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema uzinduzi wa tamasha hilo utafanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29April 2023 lenye kauli mbiu ya Zijue fursa , Imarisha uchumi , Kataa ukatili (ZIFIUKUKI) litakalofanyika katika viwanja vya leaders jijin dar es salaam.

Waziri amesema utaratibu wa tamasha hilo utakuwa ni kuwafikia jamii kwa elimu na huduma za kijamii zinazotolewa na taasisi za serikali na wadau wa meendeleo kutoka sekta binafsi.


"Kuzingatia mwitikio mkubwa wa wadau wizara imeona umuhimu wa jukwaa la pamoja la wadau wote wa maendeleo ili kuhunganisha nguvu ya kuhamasisha mwamko wa jamii kutambua fursa za kiuchumi sambamba na kukataa ukatili kwa watoto kama kampeni ya wizara ya Twende pamoja ukatili sasa Basi" amesema waziri.

Aidha waziri Gwajima ametoa wito kwa wananchi hasa jamii makundi maalumu na taasisi zote zinazolea makundi maalumu kujitokeza ili kuelimika kupata huduma na kunifunza mambo ambayo serikali na wadau wake wanafanya katika kuhakikisha uwepo wa fursa mbalimbali za maendeleo hususani kiuchumi pamoja na kuelewa mifumo inayojielekeza kwenye kutokomeza ukatili wa kinjisia kwa watoto.

Pia meongeza kuwa kupitia tamasha hilo sehemu kubwa ya jamii itazidi kuelimika na kufahamu kuhusu uwepo wa mikopo bila riba kwa makundi maalumu, huduma za mikopo mbalimbali kwa riba nafuu na huduma mbalimbali kwa maendeleo
Previous Post Next Post