Pata dhamana ya hadi 80% kutoka PASS Trust


Na Mwandishi Wetu,

Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa PASS Trust, Adam Kamanda, ameelezea fursa zilizopo PASS kwa wadau wa kilimo biashara katika kuwekeza kwenye miradi inayozingatia utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo taasisi hiyo inatoa dhamana ya hadi 80% kwenye mnyororo wa thaman katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na mazao ya misitu.

Miradi hiyo ni pamoja na inayowekeza kwenye; matumizi bora ya maji, matumizi ya nishati mbadala, matumizi bora ya ardhi, inayozingatia urejeleshaji wa taka zitokanazo na shughuli za kilimo, matumizi ya mbolea asilia na miradi yote inayozingatia kanuni na taratibu zote za uhifadhi wa mazingira.

Lengo kuu la PASS Trust ni kuhakikisha wadau wa kilimo biashara wanaongeza tija katika shughuli zao huku wakitumia rasilimali vizuri, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuleta uendelevu wa shughuli hizo.


AMESEMA KWA KIPINDI HICHO BENKI 14 ZILISHIRIKIANA NA TAASISI HIYO NA KUTOA MIKOPO YENYE THAMANI YA SHS 1.3Trioni KATIKA 66,077 NCHI MZIMA AMBAZO ZIMESAIDIA KUBADILISHA  HALI YA MAISHA YA WATANZANIA WAKIWEMO WAJASILIAMALI MALI NA WAAJIRIWA HAO NA FAMILIA ZAO.


BW KAMANDA AMESEMA KWA KIPINDI HICHO PASS IMEKUWA DARAJA MUHIMU SANA KATIKA KUWAWEZESHA WAKULIMA, WAVUVI, WADAU WA SEKTA YA MISITU, WAFUGAJI NA WAJASILIAMALI WENGINE KWENYE MNYORORO MZIMA WA THAMANI.

MKUTANO HUO ULIENDA SANJARI NA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUJANISHA MAISHA NA PROGRAMU YA UKUAJI WA KIJANI KATIKA MAISHA KWA KANDA ZA KASKAZINI.NA MAGHARIBI.


AKIZUNGUMZA KATIKA.MKUTANO HUO MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO BW NURUDIM.BABU AMBAYE ALIWAKILISHWA NA MKUU WA WILAYA YA MOSHI.BW KISARE MAKORI ALIIPONGEZA PASS KWA KUJA NA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI KUPITIA AJENDA YA UKUAJI WA KIJANI SHIRIKISHI KAMA NJIA BORA YA KUCHOCHEA KILIMO ENDELEVU

NAYE MWAKILISHI WA MKUU WA MKOA WA TABORA BW EZEKIEL MWANSASU AMEZITAKA TAASISI ZA FEDHA KUWA KARIBU ZAIDI NA PASS  ILI KUFANIKISHA MIPANGO YAKE NA KUWAKOMBOA WATANZANIA WENYE KIPATO CHA CHINI.


MIONGONI MWA WALIONUFAIKA NA TAASISI HIYO BW JEREMIA AYO WA KIJIJI CHA MBUNGUNI.WILAYA YA ARUMERU MKOANI ARUSHA AMBAYE  AMESEMA WAMENUFAIKA NA KUBADILISHA MFUMO WAO WA MAISHA KWA MIAKA 23 ILIYOPITA.

BW AYO AMESEMA KATIKA KIKUNDI CHAO WAPO WANUFAIKA ZAIDI 1000 AMBAO WAMEWEZA KUJENGA NYUMBA BORA ZA KUISHI, KUANZISHA MIRADI YA KIUCHUMI NA KUWASOMESHA WATOTO WAO HADI VYUO VIKUU NA VYUO VYA KATI NA BAADHI YAO SASA WANAJITEGEMEA.
Previous Post Next Post