WADAU WA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI KUKUTANA KATIKA MAJADILIANO YA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI


Na Lilian Ekonga, Dar es salaaak

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na Wadau katika Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imeandaa Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsiu utakaolenga kufanya majadiliano ya namna ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Naibu katibu Mkuu Uwekezaji viwanda na biashara, Ali Gugu amesema mkutano huo unatarajia kufanyika kesho tarehe 2 februari 2023 Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Julius Nyerere International Conference Centre JNICC) uliopo Jijini Dar es Salaam.


Pia amesema Mkutano huo utakua na washiriki zaidi ya 500 ukijumuisha Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Viongozi Wakuu kutoka Serikali ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waheshimiwa Mawaziri wa Kisekta, Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta, Wenyeviti wa Kongani mbalimbali, wamiliki wa kampuni, wamiliki wa viwanda, Vyama vya Sekta Binafsi, Jumuiya za Wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyabiashara wadogo na wa kati, Wakuu wa Taasisi za Serikali, watafiti wabobezi, watunga sera, washirika wa maendeleo na Asasi za Kiraia (AZAKI).  

"Kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya Taifa. Hatua hiyo, inaakisi dhamira ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kukuza na kuimarisha majadiliano na ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi" amesema Ali Gudu 

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kuimarisha Mazingira ya Biashara nchini na kuboresha upatikanaji wa miundombinu na huduma wezeshi kama vile gesi asilia, ujenzi wa reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari, umeme, maji na ardhi kwa uwekezaji.

Aidha amesema Mgeni Rasmi na Mzungumzaji Mkuu anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
 
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la biashara Tanzania TNBC, Godwill Wanga amesema Waziri wa biashra atakaa na wadau ili kuangalia namna ya kufanya sekta hii kukua katika kuangazia fursa zilizopo pamoja na kutatua changamoto.

"Tunakila sababu ya kuboresha mazingira ya biashara tukiangalia sheria, kanuni taratibu na kila ambacho kinahusu biashara huku tukikaa wadau wa sekta binafsi kujadiliana na kuona tunaenda kufika hapo tunapo tarajia kufika" amesema Wanga

Nae Mkurugenzi wa bodi ya Taasisi ya Sekta binafsi (TPSF) octavian Mshiu, amesema wakaribisha watanzania waliopo nje ya nchi kufuatilia mkutano huu kwa njia ya mtandao ili waweza kuona kinachoendelea katika maendeleo ya uchumi na biashara katika nchi yao ya Tanzania ili watusaidie kuisemea vizuri huko walipo na kuvutia wawekezaji. 

"Tunawakaribisha wafanya biashara wawekezaji, wadogo na wakubwa, wamachinga, kinamama, vijana, wakulima kwenye kongamano hilo litakalofanyika kesho"amesema Mshiu.
Previous Post Next Post