MAPATO YA NHC YAONGEZEKA KUFIKIA BIL. 257.47 KWA MWAKA 2022


Na Mwandishi Wetu,

Shirika la Nyuma la Taifa NHC limeendelea kuongeza mapato yake kufikia kiasi cha Shilingi Bilioni 257. 47  kwa Mwaka 2022 ambapo kwa Mwaka 2021 mapato ya shirika hilo yalikua ni Shilingi Bilioni 144.42

Hayo yamebainishwa Leo Jumatano Febuari 01 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Nehemia Mchechu wakati akitoa taarifa kuhusu ufanisi wa Shirika hilo kwa Mwaka 2021/2022 na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023 ambapo amebainisha kuwa mwaka 2021/2022 mapato ya Kodi yamepanda na kufikia Shilingi Bilioni 90.76 kutoka Shilingi Bilioni 89.23 
 
Mchechu amesema, mafanikio ya shirika hilo
yanatokana na maadili ya msingi sita ambayo
wamejiwekea ikiwemo weledi, ufanisi, uwazi,
ubunifu, ushirikiano na uadilifu.

"Tumewaita hapa leo kwa ajili ya kutimiza maadili
ya msingi matatu kati ya sita ya shirika. Maadili
hayo yanayotufanya kuwajibika leo kwa wateja
wetu na umma kwa ujumla ni weledi, ufanisi na
uwazi ambapo tumekuja kuwaeleza matokeo ya
ufanisi wa shirika lenu katika jitihada zake za
kuwahudumia watanzania na kutengeza faida kwa
mwaka wa fedha 2021/2022. Aidha,
nitaeleza mwelekeo wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Shirika kwa mwaka wa fedha 2022/2023,"amefafanua.

Katika hatua nyingine, Mchechu amesema, mizania
ya shirika imeendelea kuimarika na thamani ya mali
za shirika kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa na
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) zinaonyesha kuwa hadi kufikia Juni 31, 2022
zilikuwa shilingi trilioni 5.04.

Previous Post Next Post