TANESCO KUZIDI KUHAMASISHA WANANCHI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA HUSUSANI KWENYE VYANZO VYA MAJI


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema katika kuhakikisha jamii ya Watanzania wanatunza vyanzo vya maji wanatarajia kuanzisha tamasha Maalum la kuhamasisha utunzaji wa mazingira ikiwa pamoja na kupanda miti.

Akizungumza leo Januari 31,2023 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji umeme nchini ambayo imeendelea kuimarika, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema sera yao ni mazingira kama TANESCO.

Amefafanua kwenye eneo la Mazingira pamoja na mambo mengine wanahusika kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa misitu na kuhakikisha wanashughulika na shughuli mbalimbali za kuleta chachu kwa wananchi kujua umuhimu wa kutunza mazingira


“Kwa hiyo kwenye sera hiyo ni hatua ya kwanza lakini pia kwenye upande wa Menejimenti ya TANESCO nadhani mmeona juzi tulitoa ajira na tunaajiri mtu maalum kwa ajili ya kusimamia mazingira ,tunaye sasa hivi lakini tunaongeza nguvu ya timu ya mazingira ambaye ataweza kufuatilia mambo ya mazingira

“Pia TANESCO ni wachangiaji wakubwa katika mifuko ya mabonde kwa maana ya fedha kila mwaka tunalipa tozo kwenye mifuko ya mabonde ambayo fedha hizo moja ya kazi yake ni kusaidia kazi za kulinda vyanzo vya maji,”amesema Chande baada ya kuulizwa jitihada gani wanachukua kama TANESCO katika kulinda vyanzo vya maji ambavyo maji yake yanakwenda kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme.


Ameongeza wao kama Menejimenti wanafikiria kuanzisha tukio kubw la mazingira ambalo litakuwa linaleta chachu kwa wananchi kupenda kupanda miti na kutunza mazingira.

“Tunataka watu wawe wanafikiria kila mwaka kama Fiesta fulani kama Kwa mfano tunakwenda Rufiji tunaenda kupanda miti,na mwakani tunakwenda Mkoa mwingine ambako huko zitafanyika shughuli za kimazingira kwa kupanda miti.

Kwa hiyo kama menejiment tuko kwenye hatua ya kuweka Idea kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo na tutakapokuwa tayari tutashikisha vyombo vya habari kwa ajili ya kuhamasisha.

“Kama mtoto mdogo anavyojua muziki ndivyo tunavyotaka ajue na mazingira kwasababu mabadiliko ya tabianchi yako na kwenye mazingira huo ndio mpango Wetu maana sera yetu TANESCO ni mazingira.”

Akizungumza hali ya upatikanaji umeme nchini,Chande amesema mwaka jana kulikuwa na upungufu wa umeme wa kati ya megawati 200 hadi megawati 300 za umeme na hivyo Shirika lilitoa taarifa ya mipango ya kukabillana na hali hiyo kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

“Tunapenda kutoa taarifa upungufu huo umepungua kwa kiasi kikubwa na Kufanya hali ya upatikanaji wa umeme kuanza kuwa bora , hii inatokana na mipango ya muda mfupi na wa kati ambayo imekwishatekelezwa.”

Ametaja mipango ya muda mfupi iliyokamilika tayari
wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kinyerezi namba ll na umeshaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia Novemba 24, 2022.

Pia wamekamilisha matengenezo ya mitambo miwili iliyopo katika kituo cha Ubungo na
imeshaanza kuzalisha kati ya megawati 35 na 40 za umeme kwenye Gridi ya Taita kuanzia Novemba 25, 2022.Aidha wamekamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kidatu na umeshaanza kuzalisha megawati 50 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 30 Novemba 2022.

Pia tayari wamekamilisha ufungaji wa mitambo mitatu iliyopo katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi (Kinyerezi l Extension) na inaingiza megawati 120 za umeme kwenye Gridi ya Taita.

Kuhusu mipango ya muda wa kati, Chande amesema inaendelea na hivi karibuni
Majaribio ya mtambo mmoja uliopo katika kituo cha Ubungo namba l yanatarajiwa kukamilika
ifkapo mwishoni mwa Februari 2023.

Pia amesema wanategemea mtambo wa mwisho uliopo katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba 1
Kinyerezi Extension) utaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa ifikapomwishoni mwa mwezi Februari 2023.
Previous Post Next Post