WAZIRI MABULA: NHC KUKUSANYA BILIONI 5 KWA WADAIWA SUGU


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Waziri wa nyumba na maendeleo ya Makai Dkt. Anjeline Mabula amesema Katika kampeni ya miezi miwili iliyofanywa na Shirika la nyumba lataifa NHC ya kukusanya madeni kutoka kwa wadaiwa sugu wanaodaiwa malimbikizo ya kodi hadi sasa Shirika limeweza kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 5 huku akibainisha Shirika linaendelea na hatua mbalimbali ikiwemo kuingia mikataba na Wapangaji ya kuwaruhusu kulipa madeni yao kwa awamu.

Waziri Mabula ameyasema hayo  Januari 03, 2023 wakatia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu na mueleko wa utekelezaji wa masuala ya sekta ya ardhi kwa mwaka 2023.

Waziri amesema kuwa Shirika linakusudia kuvunja mikataba yaupangaji kwa waliokaidi kulipa madeni yao na kuwaondoa kwenye nyumba na kuchukua
mali zao kwa ajili ya kuuza ili kufidia madeni yao. 

"Kuendelea kukusanya madeni ya kodi ya nyumba yanayofikia shilingi bilioni 21 na madeni mbalimbali yatokanayo na uuzaji wa nyumba na viwanja yanayofikia shilingi bilioni 11.1,Msisitizo utakuwa kuhakikisha kuwa kila anayedaiwa analipa deni lake ili kuliwezesha Shirika kuendelea kuwahudumia Watanzania wote kwa kutumia rasilimali hizi za umma" amesema Waziri Mabula. 


Akizungumzia ulipaji kodi ya pango la ardhi hasa baada ya msamaha wa riba ya malimbikizo ya pango la ardhi uliotolewa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo wananchi wenye malimbikizo walipewa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo.  Waziri wa Ardhi alieleza kuwa, Kutokana na nafuu uliotolewa  Wizara yake imeweza kukusanya jumla ya shs 90,907,939,421 sawa na asilimia 75 ya lengo la nusu mwaka. 

Hadi kufikia Novemba, 2022 wananchi 2,819 wamenufaika na msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi yenye jumla ya TZS 6,946,930,272. Idadi hiyo haijumuishi wananchi waliojitokeza ambao wamehudumiwa kuanzia tarehe 1 – 31 hadi Disemba 31, 2022. 

Amewashukuru na kuwapongeza wamiliki wa ardhi waliojitokeza kunufaika na msamaha uliotolewa na Mhe. Rais na kubainisha kuwa, katika mwezi Disemba, 2022 Wizara ya Ardhi imeshuhudia idadi kubwa ya wamiliki waliojitokeza kulipa na kiasi cha bilioni 22.6 kimekusanywa katika mwezi Disemba pekee. 

Akigeukia suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi, Dkt Mabula amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia kikamilifu mipango ya jumla, mipango kina na mipango ya matumizi ya ardhi vijijini kupitia kamati za ardhi za Vijiji ili kudhibiti ujenzi holela usiozingatia mipango iliyoandaliwa na kuidhinishwa kupitia Kamati za Mipangomiji. 
Previous Post Next Post