JATU PLC YAWAHAKIKISHIA WOTE WALIOWEKEZA MITAJI NA MADAI YAO HAYATA POTEA


Na Lilian Ekonga, Jijin Dar es salaam. 

Kampuni ya Uwekezakaji ya JATU PLC imesema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha wote waliowekeza mitaji yao na madai yao hayapotei huku ikishukuru serikali ya Tanzania kupitia wizara ya kilimo kwa kuwa bega kwa bega tangu kuanzishwa kwa kampuni kwa hiyo.

Hayo yamesemwa leo January 3 na Kaimu Mkurugenzi wa JATU PLC, Mohamed Simbano alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kupokea Ugeni wa Mtaalmu wa masuala ya biashara na fedha kutoka nchini Uholanzi.

Amesema mtaalamu huyo atakuwepo nchini kwa kazi maalumu ya kusaidia kampuni kutengeneza mpango kazi mpya wa biashara itakayoendana na dira na maono ya kampuni.

"Mgeni huyu atasaidia kushauri juu ya mabadiliko ya nayoendelea na zaidi kukuza mataji kwa ajili ya kumaliza madeni yote kwa kuketi chini na wadau kuona namna ya kuendesha miradi iliyokuwepo na kuisimamia kwa waledi na ujuzi"amesema Simbano

Kwa upande wake Mtaalamu wa masuala ya Fedha, miradi na Biashara, Iyen Nsemwa amesema amefahamu mfumo wa biashara wa JATU ambao ni endelevu na utatoa mtunda kwa Wadau wake.

Ameongeza kuwa amekuja kuungana na JATU katika kuendeleza mfumo wa biashara kwa kuandaa mpango mkakati ambao ukiendelezwa utabadilisha taswira ya kampuni. 

Nae Mwenyekiti wa bodi ya JATU amesema wanaishukuru serikali na wadau wote wamehamasisha kwamba maono ya kampuni hayawezi kufutika.

"JATU inarudi kwenye mfumo sahihi sa biashara na wanaini kazi zitafanyika kwa tija na uhakiki pia tunawahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza zaid" amesema.
Previous Post Next Post