UHURU WA VYOMBO VYA HABARI HUKUZA DEMOKRASIA NCHINI


Na Mwandishi Wetu

Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini amesema, uhuru wa vyombo vya Habari hukuza demokrasia Nchini

Ametoa kauli hiyo akizungumza na baadhi ya waandishi leo tarehe 16 Januari 2023, jijini Dar es Salaam.

Amesema kukiwa na Demokrasia basi vyombo vya habari vitakua huru kwasababu sheria zitakua nzuri sio za ukandamizaji hivyo watu watakua huru kutoa mawazo na kukosoa 

Pia ametaja mambo mbalimbali ambayo yatasaidia nchi ikiwa vyombo vya habari nchini vitakuwa huru.

Amesema Serikali ina nafasi nzuri ya kuweza kujitathmini katika utendaji wao ja kuangalia kama wanakwenda vizuri au hawaendi sawa sawa.

"Vyombo vya habari ni kama kioo kwa serikali na sekta binafsi, hivyo vikiwa huru vitaweza kusaidia serikali kufanya tathmini ya utendaji kazi wake" - Sheikh Ponda
Previous Post Next Post