SHEIKH PONDA: VYOMBO VYA HABARI VIKIWA HURU MALENGO YA KUNZISHWA KAKWE YATAKUWA YAMEFIKIWA


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini amesema, vyombo vya habari vikiwa huru, malengo ya kuanzishwa kwake yatafikiwa.

Ametoa kauli hiyo akizungumza na baadhi ya waandishi leo tarehe 16 Januari 2023, jijini Dar es Salaam.

"Kama vyombo vya Habari vikiwa huru, malengo ya kuanzishwa kwake yatakuwa yamefikiwa na pia vitazidi kuaminika kwenye jamii" amesema Sheikh Ponda

Sanjali na hilo ametaja mambo mbalimbali ambayo yatasaidia nchi ikiwa vyombo vya habari nchini vitakuwa huru.

Moja wapo ya vitu alivyosema ni kuwa, Serikali ina nafasi nzuri ya kuweza kujitathmini katika utendaji wao ja kuangalia kama wanakwenda vizuri au hawaendi sawa sawa.

"Vyombo vya habari ni kama kioo kwa serikali na sekta binafsi, hivyo vikiwa huru vitaweza kusaidia serikali kufanya tathmini ya utendaji kazi wake" - Sheikh Ponda

Ikumbukwe pia wadau wengi wakiongozwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wamekuwa wakipigania mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari ili kuleta ustawi katika sekta nzima ya habari Nchini.

Na nimatarajio ya wengi hususani wadau wa habari Nchini kuwa Serikali kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye watawasilisha muswada wa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya habari mapema mwaka huu Bungeni jijini Dodoma.
Previous Post Next Post