MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AKUSANYA MILIONI 100 KWAAJILI YA KUSAIDIA WATOTO WENYE USONJI


Na Lilian Ekonga, jijin Dar es salaam

Asasi ya Kijamii Lukiza Autism Faundation imepokea hundi ya shilingi milioni 100 iliyochangisgwa na Mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka sekondari ya kimataifa ya International School of Tanganyika(IST), Madeleine Kimaro kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kutoa huduma za mazoezi tiba kwa wanafunzi wasiopungua 15 katika Kituo cha Msimbazi Mseto Ilala kitengo cha Usonji kwa muda wa mwaka mmoja.


Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mazoezi tiba katika kituo cha Usonji Msimbazi mseto ,Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism Faundation, Bi Hilda Nkabe amesema mradi huo utawasaidia watoto katika mazoez tiba ya mawasiliano na mazoezi tiba kazi.

" Milioni 100 iliyochangishwa na Mwanafunzi Madeleine ni kutokana na maradi wake umeenda na mradi wetu kuhusu usonji na kusaidia jamii kuhusiana na usonji na kutuchagua sisi na kutusaidia kutekeza mradi wetu huu wa mwaka mmoja" amesema Hilda. 

Ameongeza kuwa Mradi huo utashirikisha wataalamu wa mazoezi ambao watakuwa wakifanya kazi mda wote pia watakuwa wakiwapatia wanafunzi chakula cha mchana hapo shuleni na kutoa usafiri wa kuwafata nyumbani kuwaleta shule na kuwarudisha nyumbani kwa muda wa mwaka mmoja.


Aidha amesema Gharama za mradi huu kwa mwaka huu wa kwanza ni takribani shilingi millioni 150 hivyo amewakaribisha wafadhili wenginena na wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za
Lukiza Autism Foundation ili kukamilisha mradi huu. 

"Lengo la Lukiza Autism Foundation ni kuweza kutoa kutoa huduma endelevu kwa wanafunzi wote 45 waliopo kituoni hapo kwa sasa"amesema Hilda. 

Kwa upande wake Madeleine Kimaro amesema amechangua kufanya project ya usonji kwa sababu Tanzania usonji ni kitu ambacho kimekuwa akiongelewi sana.

"Watu wengi hawajui kama hawa watoto wanapata shida hivyo nimeamua kukusanya Milioni 100 kutoka kwa watu wengi na kuleta hapa kwa lukiza faundation ili waweza kuwasaidi watoto hawa kwa mwaka mmoja" amesema Medeleine. 

Amesema aliweza kukusanya hela kwa kuandika barua kwa kumtumia mtu mojamoja na kukusanya milioni 100 ambayo ndio yalikuwa malengo yake makubwa. 

Nae Afisa wa Elimu jijini Dar es salaam Saleh Msechu, ametoa wito kwa wazazi na wanafunzi wote kuwaleta watoto shuleni ili waweze kupata huduma hizo kuliko kuwaficha ndani.
Previous Post Next Post