MGODI WA EBR & PARTNERS WATAMBA KUNUFAISHA WANAKIJIJI


NA Humphrey Msechu, NYANG’HWALE

IMEELEZWA kuwa Mgodi wa EBR and partners uliopo katika kijiji cha Lyulu Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale Mkoani Geita tangu uanze shughuli za Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu kwenye Kijiji hicho umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa eneo hilo.

Meneja wa Mgodi huo Sunday Tumaini ameyasema hayo alipokuwa akuzungumza na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali waliotembelea mgodi huo Kwa lengo la kujifunza na kuripoti Habari zinazohusi Sekta ya madini.

Amesema kuwa kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji wa madini hayo katika eneo hilo kulikuwa na wananchi ambao pia walikuwa wanafanya shughuli hizo na kwa kuliona hilo Mkurugenzi wa Mgodi huo akawakatia kipande cha eneo kilichopo ndani ya leseni yake ili nao waendelee na shughuli ndogo ndogo za Uchimbaji kwaajili ya kujipatia chochote kuliko kuwatimua.


"Ndugu zangu wanahabari kama mnavyoona hii ni baadhi ya mitambo ambayo tunaitumia kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu hapa na kwakweli Mgodi huu umekuwa na tija sana hususani kutokana na uzalishaji wake kwani wananchi wameweza kupata ajira lakini pia Serikali imekuwa ikifaidika na kile ambacho linatoka hapa."amesema Tumaini

Alisema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni miundombinu ya barabara na umeme hivyo anaiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iweze kuwasaidia kutoboreshe miundombinu ya barabara na pamoja na umeme ili waweze kufikisha madini yanayochimbwa Sokoni".Amesema


Ameongeza kuwa umeme utawezesha kuongeza uzalisha kwa tija na serikali kuendelee kunufaika kutokana na uwekezaji wao kwa kuweza kutoa mirahaba mikubwa na hata wananchi wanaozunguka eneo la mgodi nao waweze kunufaika kupitia mgodi huo.

Katika hatua nyingine wanamshukuru Afisa madini mkazi (RMO) wa mbogwe kwa ushirikiano mkubwa anaowapatia ukiwemo ushauri mzuri ambao kimsingi unawasaidia kwenye shughuli zao mfano uliwezesha kukaa na mkurugenzi nakuona Kuna umuhimu wa kuwapa wanakijiji leseni ya Iparan'ombe ili weweze kuchimba.


Amefafanua kuwa wachimbaji hao wadogo waliwapa utaratibu wa uchimbaji mdogo wa madini kuwa watakuwa wanakatwa mawe wanayokuwa wamepata kupitia uchimbaji wao ikiwemo asilimia za mraaba wa serikali na mawe mengine yanabaki kwa muwekezaji.

Ameongeza kuwa na asilimia nyingine wanayopata wanarudisha kwenye jamii inayowazunguka hivyo wao wanachukua asilimia 30 na wachimbaji wanachukua asilimia 5 ila wanapata manufaa makubwa kupita uwepo wa mgodi huo kwasababu kwenye duara moja wanatoa mifuko ya mawe zaidi ya 400 na maduara yapo zaidi ya 20.

Akizungumzia faida za uwepo wa Mgodi huo Tumaini amesema kuwa wamesaidia kutengeneza barabara kiwango cha changarawe kutoka Wilayani mpaka katika Kijiji hicho ambako kuna uwekezaji wa Mgodi.


“Kama mgodi bado tupo karibu na wananchi kwenye shughuli za maendeleo ambapo katika siku za hivi karibuni tumeweza kusaidia kuezeka shule ya Msingi Bea baada ya kuezuliwa na upepo na kuharibu paa ambapo uongozi wa kijiji ulikuja kuomba msaada Mgodini pamoja na mambo mengine,” amesema.


Previous Post Next Post