BENKI YA MAENDELEO YAPATA FAIDA MARADUFU MWAKA 2021 KUTOA MILIONI 580 HADI BILION 1


Na Lilian Ekonga, Dar es salaaam

Licha ya changamoto zilizojikeza za kiuchumi mwaka 2022 ikiwemo janga la Uvicko-19, Benki ya Maendeleo imefanikiwa kupata faida ya shilingi bilioni 1.3 kutoka shilingi milioni 580 mwaka 2021 huku ikitaraji kuwafikia zaidi ya Watanzania 7000 wakiwemo wanawake na vijana kuwapatia elimu ya usimamizj wa fedha pamoja na mikopo.

Kauli hiyo imetolewa Leo january 30 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt Ibrahim Mwangalaba wakati akitoa tathmini ya ukuaji wa benki hiyo mwaka 2022.

Amesema kuwa 2022 benki hiyo pia imesajili ukuaji wa faida kwa asilimia 184 huku sababu zilizchongia kukua ni pamoja na ukuaji wa njia za uzalishaji huku akisema kuwa amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 11 kutoka shilingi bilioni 70 hadi bilioni 77 mwaka jana.

Katika hatua nyingine Dkt Mwangalaba amesema mwaka 2022 benki ya maendeleo imefanikiwa kutoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa wamachinga zaidi ya 2500.

Aidha benki hiyo imeendelea kujihimirisha katika huduma za teknolojia kwa kutambulisha thamani ya bidhaa za kidigitali ikiwemo benki mtandao, mfumo wa ukusanyaji wa malipo –PCS hatua iliyotajwa kuongeza faida kwa wanahisa kufikia zaidi ya asilimia 10.
Previous Post Next Post