BALILE: SHAUKU YA WADAU WA HABARI NI KUONA MUSWADA YA SHERIA YA HABARI UKIWASILISHWA BUNGENI


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Muswada wa Sheria ya Habari kuwasiliswa Bunguni mwezi huu kama ambavyo serikali ilitoa ahadi yake mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza leo Januari 19,2023 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Deodatus Balile, amesema mwelekeo ni mzuri na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa na shauku wa wadau wa habari kuona mswada huo unaingia bungeni.

" Wiki hii tunarajia kwamba Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari itawasilisha muswada wa  huduma za habari bungeni na utajadiliwa na mungu akipenda mwezi Febuari utakua umepitishwa kuwa sheria na tumeona kwamba mweleke ni mzuri " amesema Balile 

Wadau wa habari wana shauku kubwa ya kusikiliza muswada wa sheria ya habari ukisomwa kwa mara ya kwanza katika Bunge la Januari hii.

Amesema kuwa mwezi huu wanatarajia kwamba Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itawasilisha muswada wa huduma za habari bungeni kama waziri alivyoahidi (Nape Nnauye) mara kadhaa kwamba utaingia bungeni na kujadiliwa.

“In sha Allah Mungu akipenda mwezi Februari itakuwa imepitishwa na kuwa sheria basi tutaanza utaratibu mwingine wa kuunda vyombo vinavyotakiwa ikiwemo Baraza Huru la Habari, na utunzi wa kanuni zitakazokuwa zimetokana na mabadiliko mbalimbali” amesema.

“Tunaona mwekelekeo ni mzuri na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa sasa na hamu yetu kubwa ni kuona muswada huo unaingia bungeni baada ya kushindikana katika Bunge la Februri mwaka jana,ukashindikana mwezi wa tisa,ukashindikana mwezi wa 11 .

“Lakini sasa tulishazungumza na Waziri,watendaji wa serikali ni matumaini yetu makubwa sana sana tunataraji kuona mswada huo ukiingia bungeni na mambo yote yaweze kwenda vyema,” amesema.
Previous Post Next Post