Kamishna Mkuu wa chama cha Skauti Tanzania ametangaza kumaliza muhula wa uongozi wake wa miaka minne


Na Lilian Ekonga, jijini Dar es salaaam. 

 Kamishna Mkuu wa chama cha Skauti Tanzania Bi Grace Kado ametangaza kumaliza muhula wa uongozi wake wa miaka minne tangu alivyoanza mwaka 2018 huku shughuli zote chama zikitekelezwa na Naibu Kamshina Mkuu mpaka Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan atakapokamilisha safu ya Uongozi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo January 21 Jijini Dar es salaam, Grace Kado amesema yeye atabaki kuwa mwanachama na Mkufunzi Msaidizi wa chama cha Skauti Tanzania kufuatia katiba ya chama ibara 10.6.1(iii).


"Napenda kuwaambia Skauti wenzangu ya kwamba chama bado kipo katika wakati amabao unahitaji zaidi mshikamano na hekima kubwa katika kutekeleza shughuli zetu"amesema Grace

Aidha Bi Grace amewapongeza skauti wote Tanzania kwa kuendelea kuonyesha ukomavu na busara kubwa katika kujadili, kuamua na kutekeleza jambo lolote ambalo wanaliona linakiuka taratibu zao. 

Ameongeza kuwa katika kipindi cha Uongozi wake aliweza kuwasaidia vijana katika maswala mazima ya maadili na vijana wengi wameweza kuwa na maadili mema.


Nae Naibu Kamishna Mkuu wa chama cha Skauti Abubakar Mtitu, amesema kwa kushirikiana na wenzake watasimamia misingi ya Skauti na kwa kutumia wajibu wangu binafsi kwa kufanya maamuzi ya misingi ya skauti kwa kutatua migogoro katika kipindi hichi cha kusubiri.
Previous Post Next Post