MEENA: MABADILIKO YA SHERIA NA SERA YA MWAKA 2023 YATAATHIRI SERA ILIYOPO


Na mwandishi wetu

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema kuwa Mabadiliko yanayofanywa kwenye Sheria na sera ya mwaka 2023 lazima yataathiri Sera iliyopo sababu ya katiba iliyopo.

Akizungumza na Waandishi wa habari meena alisema kuwa sheria yoyote ikitofautiana na sera,hulazimika kubadilishwa ili kukidhi haja ya sheria.

Meena alisema kuwa Kuna sheria ya habari ambayo inatarajiwa kupelekwa bungeni mwezi wa kwanza 2023 kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho hivyo ni muhimu kuzingatia sera ya habari


“Kimsingi Mabadiliko yanayofanywa kwenye Sheria lazima yaathiri Sera iliyopo sababu haiwezi kukiuka Katiba na Sera “ amesema Meena.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile amesema sera hiyo kurekebishwa, serikali na wadau wataangalia namna ya kuwa na sheria moja ya vyombo vya habari, badala ya kuwa na sheria zinazosimamia tasnia hiyo.

" Hizio sheria nyingine bado sababu tulitaka tupambane na ajenda moja hiyo sheria ya huduma za habari ishakwenda hizi nyingine Waziri wa habari amekuja na wazo ya kwamba tukishamaliza sheria ya habari tuanze mchakato wa mabadiliko ya sera ya habari maana sera tuliyonayo ni ya 2003" amesema Balile 
Previous Post Next Post