TIC YASAJILI MIRADI 132 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA DOLA BILIONI 3.16


Kituo cha Uwekezaji Tanzanzia (TIC) kimesajili jumla ya miradi 132 sawa na ongezeko la asilimia 22.2 ikilinganishwa na miradi 108 iliyosajiliwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba 2022 mbapo Sekta ya Viwanda imefanikiwa kuongoza kwa kuvutia miradi mingi (67).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, John Mnali alisema Ongezeko hilo kubwa la Miradi iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji linatokana na Jitihada za Serikali za Kutangaza fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizoko nchini Tanzania kupitia Ziara mbalimbali za Viongozi wa Kitaifa nje ya nchi pamoja na juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Mnali alisema mbali na sekta ya viwanda, sekta nyingine mbalimbali zilifuata kwa kuvutia miradi mingi ikiwemo Sekta ya Usafirishaji miradi (25), Utalii miradi (12), Kilimo (9), Huduma (8), Majengo ya Biashara (7), Rasilimaliwatu (3) na Sekta ya Fedha (1).

Mnali alisema Miradi hiyo ina jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3.16 na inatarajiwa kutoa ajira 21,297.

"Thamani ya miradi (USD bilioni 3.16) iliyosajiliwa katika kipindi cha Julai – Novemba 2022 imeongezeka kwa asilimia 259 ikilinganishwa na thamani ya miradi (USD milioni 881) iliyosajiliwa katika kipindi cha Julai - Novemba 2021."

Aidha Mnali alisema Kati ya miradi hiyo, miradi ya 50 inamilikiwa na wageni (foreigners) wakati Miradi 30 inamilikiwa na Watanzania (locals) na miradi 52 inamilikiwa kwa ubia kati ya watanzania na wageni (Joint ventures).

Mbali na hayo Mnali alisema kufuatia usajili huo kiwango cha ajira mpya kinatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 57.

"Kiwango cha ajira kinachaotarajiwa kutokana na miradi iliyosajiliwa Julai – Novemba 2022 kimeongezeka kwa asilimia 57 kutoka ajira 13,578 (Julai – Novemba 2021) hadi ajira 21,297 (Julai - Novemba 2022)."

Previous Post Next Post