HOSPITALI NCHINI ZAANZA KUZALISHA MAZAO YA DAMU

Kaimu Meneja Mpango wa Taifa Damu Salama Dkt. Abdul Juma akiongea na waandishi wa habari(hapo pichani) kuhusu kampeni ya uhamasishaji wa uchangiaji wa damu salama kwa kushirikiana na UFM ya Azam Media.


Na. Catherine Sungura, WAF,Das es Salaama

Hospitali za Rufaa za Mikoa,Halmashauri na Taasisi za Wizara ya Afya kuanza kuzalisha mazao ya damu wakati wa uchangiaji damu salama.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Abdul Juma wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea Kampeni ya uhamasishaji uchangiaji wa damu salama kwa kushirikiana na Kituo cha Radio cha Uhai Fm chini ya Azam Media.

Dkt. Juma amesema hivi sasa mazao hayo ya damu yanazalishwa moja kwa moja wakati mtu anapochangia damu kulingana na mahitaji ya kituo.

"Uzalishaji huu unatokana na uwezeshaji  wa Serikali ya Awamu ya Sita kununua mashine za kisasa aina ya ...ambayo humuwezesha mchangia damu kuchangia zao la damu kulingana na mahigaji ya wakati huo"Amesema Dkt. Juma

Aidha, amesema mahitaji ya sasa ya yamefikia asilimia 76 ambapo Wizara ya Afya imeweka malengo ya kukusanya chupa 550,000 za damu ambayo ndio mahitaji ya nchi kwa Mwaka.

Kwa upande wa mashirikiano hayo Dkt. Juma amesema kituo cha Radio Uhai FM  na kampuni na AM Creative watafanya uhamasishaji kwa jamii wakati wa ratiba za uhamasishaji uchangiaji damu salama  nchin nzima pamoja na shughuli za Kitaifa kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza na Iringa.

Naye, Mhariri Mkuu wa Radio Uhai FM Bw. Ramadhani Tuwa amesema wameamua kuhamasisha uchangiaji damu salama kupitia Radio yao kwani wamekuwa wakiripoti matukio mengi yenye uhitaji wa damu hivyo wameona vyema kushirikiana Serikali kutoa elimu.
Previous Post Next Post