NIT YASHAURIWA KUBORESHA MITAALA ILI KUENDANA NA SOKO LA AJIRA


Na Lilian Ekonga. 

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini NIT kimeshauriwa kuendelea kuboresha mitaala ya mafunzo chuoni kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya usafirishaji ili kuzalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira kutokana na kukua kwa sekta hiyo nchini pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia. 

Ushauri huo umetolewa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Usafirishaji nchini TSC Sallu Johnson wakati wa ufunguzi wa Tamasha la taaluma liitwalo Career Fair lililoandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi katika kukabiliana na hali ya soko la ajira nchini.

"Chuo Kikuu cha usafirishaji nchini kiendelee kuboresha mitaala ya mafunzo vyuoni kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo ili kuendana na soko la ajira za wataalamu nchini."amesema Sallu


Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Profesa Zakaria Mganilwa amesema tamasha hilo limewakutansha wadau wa sekta za usafirishaji na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo pamoja na kupata uelewa wa soko hali ya soko la ajira nchini.
 
Aidha Mkuu wa Chuo hicho amesema tamasha hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika uboreshaji miundombinu ya usafirishaji ikiwemo ujenzi wa reli, ujenzi wa bandari pamoja na ujenzi wa meli kwa kuwaandaa wataalamu wazawa waliobobea katika sekta hiyo.


Hata hivyo nao baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema matokeo ya tamasha hilo ni kujenga mahusiano na waajiri pamoja na kupata uzoefu wa mahitaji ya soko la ajira hasa ili kuendana mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Previous Post Next Post