Na Humphrey Msechu, Karagwe
MKUU wa Chuo cha Veta Wilaya ya Karagwe Pascal Thomas amesema serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa chuo cha Veta kilichopo Mkoani Kagera.
Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inapanua wigo mpana wa huduma zake katika kuwekeza kwenye vyuo vya ufundi vya wilaya , ambapo hapo awali kulikuwa na vyuo vya mkoa na vyuo vingine vilikuwa kwenye kanda.
Ameyasema hayo leo desemba 5, 2022 mkoani Kagera Mkuu wa Chuo cha Veta Wilaya ya Karagwe Pascal Thomas licha ya serikali kutoa zaidi ya bilioni 4, wanamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutoa bilioni 1.3 ya kununua vifaa na mitambo katika kalakana na kuwafadhili wanafunzi wapatao 109 wasio na uwezo kusoma kozi za miezi sita na sasa hivi vijana hao wanaelekea kuhitimu masomo yao.
“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyowezesha Chuo cha Veta wilayani karagwe ,chuo cha Veta karagwe kinauwezo wa kupokea vijana 250 kwa kozi ndefu lakini hata hivyo kinazo kozi fupi fupi ambazo zinaendeshwa chuoni hapo
" na zaidi ya vijana 450 ambao tunaweza kuwapokea kwa mwaka hivyo uwezo wake hadi hivi sasa ukiweka kozi ndefu na fupi inamaana karibu vijana 700 wanaweza kupokelewa na mpaka sasa tunao vijana 250 ambao wanategemea kufanya mtihani wa taifa ambao wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili.”amesema Thomas
Na Kwaupande wake mwanafunzi wa chuo hicho David Adam ambaye anasoma kozi ya muda mfupi ( DMO) ambayo imedhaniwa na ofisi ya Waziri mkuu na mafunzo yao yameanza Juni sita mwaka huu na wanamalizi Disemba 12 mwaka uhu na kozi hiyo ililenga mafunzo ya ufundi stadi wa kozi mbalimbali ikiwamo Umeme.Selemala, Fundi magari .Uwashi., na ujenzi hivyo wanatoa shukrani kama watanzania ofisi ya Waziri mkuu kwa kudhamini mafunzo hayo kwani wengine walikuwa hawana uwezo wa kugharamia mafunzo hayo.