Na lilian Ekonga. Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ametoa onyo kwa wasimamizi wote wa mitihani na watumishi wa serikali kuanzia ngazi za maafisa Elimu wa mikoa, wilaya na walimu wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa mtihani wafungwe na wakae ndani hata kwan miez sita tuu lakini wasipigwe faini ili ije kuwa fundisho kwa wengine.
Waziri ametoa kauli Hiyo leo Disemba 5 jijini Dar es salaam, ambapo amesema watapitia sheria zao na kuhakikisha kwamba kama kuna upenyo unaowezesha watu wafanye udanganyifu kwenye mitihani na wakatoka bila kuchukuliwa hatua yoyote watapeleka mapendekezo ya kufanya mabadiliko ili yoyote anayechezea mtihani wala asipigwe faini afungwe jela.
Waziri Mkenda amesema kuwa Wataongea na mamlaka husika kwamba wasiwe wanawafukuza tuuh kazi bali wanachofanya ni kitendo cha jinai na ukiangalia garama za kuendesha mitihani ni kubwa sana na mtu anayevuruga mitihani anahujumu uchumi wa nchi yetu.
"Nisisitize kwamba kuna kauli inasema ukitaka kuua taifa ua Elimu haribu elimu ya nchi ile, Na sasa hivi tunafanya mageuzi ya elimu hapa nchini sera mitaala haiondoi jukumu la kusimamia kwamba elimu tunayoitoa sasa hivi tunaitoa kwa tararibu zinazo kubalika sio kwa mtu kwenda kufanya udanganyifu katika mitihani."amesema prof Mkenda.
Ameongeza kuwa wataendelea kuongea na mamlaka kwamba watu hawa wachukuliwe hatua kwa kuwafukuza kazi au kuwasimamisha kazi washitakiwe mahakamani wahukumiwe na waende jela.
"Waache kufundisha watoto rushwa, udanganyifu na taifa letu halita endelea kwa kuwafundisha watoto wetu udanganyifu na swala la mitihani hawata kuwa namchezo nalo wataendele kukaza buti na wanaopanga kufanya hivyo wajue kwamba watawakanata tuu."amesema Waziri
"Tutaendelea kuongea na mamlaka kwamba watu hawa wachukuliwe hatua kwa kuwafukuza kazi au kuwasimamisha kazi washitakiwe mahakamani wahukumiwe na waende jela,"amesema.
Amesema udanganyifu huo unatokea pale kwenye kituo cha kufanyia mitihani mara nyingi na wameweza kunasa shule mbali mbali ambopo wasimamizi pamoja na walimu wa pale wameshirikiana kwa namna moja ama nyingine kufanya udanganyifu katika mitihani.