Na Lilian Ekonga, jijini Dar es salaam
Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya viwanda ikiwa na pamoja kuimarisha upatikaji wa nishati ya umeme wa uhakika na kwa bei nafuu, kujenga barabara , reli na viwanja vya ndege, bandari na miundombinu mengine ya uchuzi ili kuweza kukuza wizara ya biashara.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya viwanda Zanzibar, Mhe Omar Said Shaaban wakati akifungua Maonesho ya Saba ya Bidhaa za viwanda vya Tanzania yanofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 3 Disemba hadi 9 yanoratibiwa na Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania(Tantrade).
Waziri amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia tantrade katika kutekeleza majukumu yake ili waweze kuongeza kasi zaidi ya kuendeleza na kukuza biashara nchini.
"Naagiza tantrade kushirikiana na idara za biashara nchini zilizipo katika ofisi zetu za tawala za mikoa katika kuwafikia wenye viwanda kwa lengo la kuwaunganisha na masoko kutoa programu za uendeshaji na ukuzaji biashara na fursa mbalimbali zilizopo nchini" amesema waziri Omar.
Aidha ametoa wito kwa wasomi na watafiti kufanya tafiti zitakazo saidia viwanda nyetu kuimarika kwa kutumia mazingira halisi ya Kitanzania.
Pia waziri ametoa wito kwa washiriki wa maonyesho hayo kuyatumia ipasavyo ili kuweza kutangaza technolojia ya viwanda vidogo, vya kati na viwanda vikubwa.
"Nimefarajirika sana tantrade imefanya jitihada za kuwaanganisha wazalishaji na technolojia ufunganisha wa bidhaa na kuratibu misafara ya kibiashara katika wa nchi mbalimbali" amesema Waziri
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Bi Latifa Khamisi amesema maonyesho hayo yanakutanisha wadau 502 katika sekta za uzalishaji , kilimo, uvuvi, mifugi na bidhaa za viwandani za technolojia mbalimbali.