200 KUPELEKA UJUMBE WA UHURU KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO


Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.

Zaidi ya Watanzania 200 likiwemo kundi la Mabalozi wanatarajia kuianza safari ya siku sita ya kupanda Mlima Kilimanjaro kuelekea kilele cha Uhuru ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 tangu Tanzania ipate Uhuru.

Safari ya upanda Mlima itatanguliwa na hafla fupi ya kuwaaga wapandaji hao katika Lango la Marangu,hafla itakayoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt.Pindi H.Chana(Mb)
 
Miongoni mwa Mabalozi wanaopanda Mlima huu ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Dkt. Asha Rose Migiro ambaye ataongoza kundi la mabalozi kupanda kilele hicho kirefu zaidi Afrika.
Previous Post Next Post