Waziri Biteko aipongeza NSSF kwa kuwafikia wachimbaji wadogo wadogo wa madini


Na Humphrey Msechu

WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amewapongeza mfuko wa Taifa wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) kwa kutekeleza mpango wake wa kuyafikia makundi mbalimbali haswa kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini Katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati alipotembelea kwenye banda la NSSF katika Maonyesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya uwekezaji (EPZA) Bombambili Mkoani Geita, Waziri Dotto Biteko amewapongeza NSSF kwa mchango wao katika sekta ya madini nchini.


Waziri Biteko ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unavyohakikisha unatekeleza mpango wake wa  kuyafikia makundi mbalimbali yakiwemo ya wachimbaji wadogowadogo wa madini katika maeneo mbalimbali.  

Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele amemuhakikishia Waziri wa madini Dkt. Dotto Biteko kuwa wataendelea kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wapo ikiwa pamoja na kusajili wanachama wapya wanaofika katika maonyesho ya madini nchini. 

NSSF inashiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa huduma mbalimbali za Hifadhi ya Jamii kwa wanachama na wananchi ikiwa pamoja na kusajili wanachama wapya wanaofika katika Banda la NSSF.  
Previous Post Next Post