WAKAZI WA BUGURUNI KISIWANI WALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUDHIBITI PANYA ROAD


Na mwandishi wetu

Wakazi wa Buguruni Kisiwani, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaa, wamelipongeza jeshi la Polisi katika jitihada zao za Operesheni za kuwakabili Wahalifu hususani ni Panya Road, ambao wamekua wakihatarisha maisha yao.

Wananchi hao wamesema hayo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika Shule ya Msingi GANA ambapo walitoa maoni yao kuhusiana na namna Jeshi la Polisi walivyojitoa kupambana na Panya Road.


Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Omari Kumbilamoto amewaambia sababu kubwa ya kuwepo PanyaRoad ni wazazi kuowasihi watoto wao kusoma licha ya jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye utoaji wa Elimu Bure, hivyo amewataka kumuunga mkono Rais Samia kuitikia wito wake wa kuwapeleka shule.

Nae Mwenyekiti wa Mtaa Kisiwani , Bw Uwesu Bakari Uwesu amesema anaishukuru jeshi la Polisi Kwa kuweza kukabiliana na Wahalifu hususani watu wanaojihusisha na vitendo vya unyanganyi Kwa kutumia silaha (Panya road)

Pia amewaomba wananchi waweze kutoa Ushirikiano wa kutosha na Serikali za Mitaa pamoja na jeshi la polisi Ili kuhakikisha Hali ya Usalama inazidi kuimarika Katika Mtaa wa kisiwani.


"Wazazi wamekuwa wakilalamika kuhusiana na kukamatwa Kwa watoto wao, tunatakiwa tujifunze Hayo Mambo yanasikitisha sisi tunataka watoto wenye maadili mazuri"amesema Mwenyekiti.

Kwa upande wake mkazi wa kata ya Kisiwani amsema wanalishukuru jeshi la Polisi Katika kuwathibiti na Panya road ambao walihatarisha Hali ya kiusalama Katika Mtaa wao wa Kisiwani.
Previous Post Next Post