TANTRADE YATOA TATHIMINI YA MAONYESHO YA SABASABA YALIYOFANYIKA JULY MWAKA HUU


Na Humphrey Msechu


KAIMU mkurugenzi  mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Tantrade  Twilumba Mlelwa Amesema kuwa maonyesho ya 46  Jukwaa la kimataifa la biashara Dar es  Salaam DITF yalikuwa na mafanikio makubwa sana ikiwa na ongezeko la shiriki na watembeleaji ambapo jumla ya kampuni 3200 za kitanzania na 225 kutoka chi 23 za Afrika ,Asia ,Ulaya pamoja na Marekani ya kesini zilishiriki katika maonyesho ya maka huy 2022 ukilinganisha na Kampuni 2926 za kitanzania na kampuni 76 kutoka nchi 17 maka 2021.


Amesema kuwa pia kulikuwa na watembeleaji 350000 na mikataba iliyosainiwa Tisa Kenye thamani ya Tsh.Bilioni 176 na mpango ulioandaliwa za Bussines Kliniki ,Industrial Solution ,B2B,watoto urithi wetu huduma ya afya,benki,Nida,Polisi,Lita,Uhamiaji pamoja na Dart.


Twilumba Mlelwa ameyasema  hayo katika mkutano uliowakutanisha wadau wamaonyesho katika ukumbi wa sabasaba jijini Dar es Salaam jana ,ambapo alisema kwakutambua umuhimu katika maonyesho Tantrade iliunda timu ya wataalam kufanya tafiti wakati wa maonyesho hayo ya 46 ya jukwaa la kimataifa la biashara Dar es Salaam 2022 kwa lengo la kuangalia jinsi gani washirika wanavyonufaikna na maonyesho ikiwemo ubora ,huduma,kukuza bidhaa .ulinzi pamoja na usalama.

  


Alisema katika utafiti huo maoni mbalimbali yalipokelwa na Tantrade ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa upangishaji mabanda hususani kwa watu wenye ulemavu ,tatizo la ukatikaji wa umeme mara kwa mara hasa kwa shiriki waliokuwa na maturubai  ya wanyama ,na mikumi .EOTF, Taaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na hivyo kusababisha baadhi ya vifaa vya washiriki kupata itilafu kutokana na katizo la mara kwa mara la meme.


Aliongeza kawa changamoto nyingine ilijitokeza ni kuchelewa kwa vitambulisho kwa wadau na kusababisha baadhi ya washiriki kulipa viingilio mlangoni kulikochangiwa na kuchelewa kuthibitisha ushiriki,washiriki kutokuzingatia kanuni za ushiriki,ikiwa pamoja na kuingiza magari tao nani ya uwanja,na baadhi ya Mabanda kutokuwa tayari kwa wakati uliopangwa ,matumizi makubwa ya sauti ya mziki na ngoma hivyo baadhi ya washiriki kutokuwa na usikivu wa kutosha.



Mlelwa akisoma tariifa hiyo kwaniaba ya Kaimu Mkurugenzi Idara ya ukuzaji biashara Tantrade Fortunatus Muhambe .alifafanua kuwa uchakavu wa miundombinu ya maonyesho ,na kupelekea kuwa na gharama kubwa ya matengenezo ikiwemo vyoo,na mavumbi katika maeneo ya maonyesho,gharama kubwa ya chakula kwa washiriki,hasa waliokuwa wametoka nje ya chini na hiyo nikutokana na kutoelewa rugha ya Kiswahili.


Aliongeza kuwa tafiti hiyo ilionyesha kuwepo kwa hali uwiÄ™zi kaika baadhi ya mabanda,uwepo wa foleni kwenye Milango ya kuingilia uwanjani iliyosababishwa na huduma ndogo ya ‘’scanning’’, na huduma hafifu ya mtoa huduma ya mizigo kwa nia ya mikokoteni na kwa kumalizia niwahakikishie kuwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tantrade itahakikisha inayafanyia kazi maoni yote ambayo kimsingi yanalenga kuboresha maonyesho yajayo “Tutahakikisha kwamba yanafanyiwa kazi kikamilifu ili maonyesho yajayo yawe na tija stahiki katika kupata masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali hususani zinazozalisha hapa nchini.”alisema Mlelwa.



Akizungumzia mikakati  ijayo ya kuboresha miundombinu alisema kuwa watahakikisha wajenga vyoo,vya kisasa 20,ugawaji wanafasi za kieletrioniki,kuratibu mikutano ya kibiashara,kutoa matangazo ya kuhamasisha ushiriki na watembeleaji mapema  na kupanua wigo wa kushirikiana na sekta binafsi katika kuratibu na kutoa huduma mbalimbali kwenye maonyesho pia wataendelea kusimamia vyema taasisi ili kuhakikisha sekta ya biashara nchini inaendelea kutoa mchango katika ukuaji wa schumi wa taifa,na kusimamia na kuboresha zaidi maonyesho kwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto zikiwemo za kimfumo wa kiutendaji.



Previous Post Next Post