MFUMO WA LUKU KUTOFANYA KAZI KWA SIKU NNE



Shirika la Umeme Tanzania limetangaza kufanya matengenezo hayo kwenye Kanzi Data ya Mfumo wa manunuzi ya Umeme (LUKU) ili kuongeza ufanisi

Matengenezo hayo yatachukua Siku 4 kuanzia Jumatatu ya Septemba 12 hadi 15, 2022 na wateja wataweza kununua Umeme muda wote isipokuwa kuanzia Saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi




Shirika limeshauri wateja kununua Umeme wa ziada au kufanya manunuzi nje ya muda wa matengenezo ili kuepusha kukosa huduma. 
   


Previous Post Next Post