MCHUNGAJI MATATANI KWA KUMBAKA MUUMINI ALIYEZIMIA



Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Amani Upendo, Mchungaji wa Kanisa la Siloam lililopo Kijiji cha Manda Chini, kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wakati akimfanyia maombi

Tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 30, 2022 wakati binti huyo anayedaiwa kusumbuliwa na matatizo ya kuanguka alipokwenda kwenye Maombi na Watu wengine ambao Mchungaji huyo aliwaagiza wamuache akifanyiwa maombi kipekee 
-
Baada ya kuachwa, Mtuhumiwa anadaiwa kumuombea Binti huyo na alipoanguka alitumia nafasi hiyo kumuingilia Kimwili na alipozinduka aligundua amefanyiwa Unyama huo.


Previous Post Next Post