Tume ya Madini inawakaribisha wadau wa madini na wananchi wote kutoka katika Mkoa wa Geita na mikoa mingine nchini kwenye banda lake lililopo kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita.
Elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.
Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.
Pia tunatoa huduma ya usajili wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastral Transactional Portal) na upimaji wa madini ya metali.
Nyote mnakaribishwa.