Sigara yenye nembo ya biashara ya Supermatch kutoka nchi ya Congo, iliyokamatwa baada ya kuingia nchi
Na. Mwandishi Wetu,
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA),Kanda ya Ziwa Magharibi imekamata bidhaa za tumbaku aina ya siagara bandia zenye thamani ya Bilioni 1.8, zilizotokea nchi ya Congo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TMDA, zimebainisha kuwa: Baada ya kupokea taarifa ya kontena lenye bidhaa za tumbaku lililozuiliwa katika ofisi ya TRA Shinyanga, imebaini kuwa sigara hizo ni bandia na zimeingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Kongo
ambapo kuna makasha 2200 yenye thamani ta TZS 1.8 Billioni na uzito tani 13.2." Ilisema taarifa hiyo.
Hatua zaidi zinaendelea mzigo umezuiliwa" Ilimalizia taarifa hiyo.