HAJI MANARA AITOLEA UVIVU TFF



Anaandika HAJI MANARA 

Hata haieleweki kimejibiwa kitu gani?
Na kwa nini Issue ya Yanga uharaka wa kujibu unakuwa mkubwa mno?

Kanuni hizi  hizi zilizombadilisha Chikwende Kwa Kahata ?
Kanuni hizi hizi zilizomhalalisha Kibu kucheza bila kupata uraia?
Au mnazungumzia zipi ndugu zangu?

Kazi yenu na kusaidia Wachezaji wacheze mpira na sio kuwazuia na ndio maana bila baraka zenu ITC ya Kisinda isingepatikana na faini alilipishwa nani?

Last season tena kwa maksudi,Yanga pamoja na kuomba kucheza na Washabiki kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa,hamkupeleka barua CAF.

Matokeo yake Club ikakosa mapato mengi kwenye mchezo dhidi ya Rivers ya Nigeria,na sio mapato tu ,kucheza bila mashabiki nyumbani kunaweza kuchangiwa na kutolewa mapema kwenye Mashindano yale.

Wiki hiyo hiyo wenzetu Team Pendwa walicheza na Washabiki wao.

TFF kanuni kuwa favoured ni kwao tu ila Kwa Yanga zinavunjwa?



Mbona hamkuwahi kujibu kuhusu kuwanyang’anya Yanga haki ya kucheza bila mashabiki?
Ktk muktadha wa Utawala Bora,, kosa kubwa kama lile ktk Mashirikisho mengine,angebaki mtu hapo?
Nani aliwajibika?

Hv ile Issue ya kahata na hii utofauti wake upo ktk kanuni zipi?

Halaf mnaendelea kuwatumia Wanaharakati wenu wale wale wa kila siku kusema Yanga inaichafua TFF,,kwa hyo mlitaka tukae kimya?  Ahh nimesahau nyie ni MAMLAKA 

Naendelea kuwakumbusha, Yana mwisho haya 🙏🏻🙏🏻

#Bugati  

Previous Post Next Post