UZINDUZI WA KAMPENI YA MZIGO SIO UTANI, BEI MPYA YA KISIMBUZI CHA AZAM TV KINACHOTUMIA ANTENNA.




Katika kukidhi haja ya kiburudani kwa wateja wao nchini Kampuni ya Azam limited yaongeza Mikoa 6 ya kuhakikisha wanapata Huduma ya kiburudani, Michezo na Habari.

Akizungumza na waandishi wahabari Afisa Mtendaji MKuu kutoka Azam Tv  Loth Mziray , amesema mara baada ya kutambulisha Mikoa 6 ikiwemo Lindi,Tunduru,Kigoma, Sumbawanga,Makambako pamoja na Tabora amesema katika kuendeleza na kukuza burudani bila kuleta utani nchini.

Hata hivyo Mziray ameongeza kuwa ongezeko la mikoa hiyo 6 ni kutokana na kuhakikisha nchi nzima inabeba dhima ya ''Azam tv sio utani" na kuwafikia wateja wao nchi nzima.

Pia ameeleza kuwa kutokana na kuongeza kwa mikoa hiyo wameamua kushusha bei ya kupata visimbuzi hivyo Ili kuwapa nafasi watu wa hali ya chini kuvipata ikiwemo visimbuzi vya antena kwa bei ya 79,000 badala ya 99000 Huku 59000 badala ya 85,000 kwa visimbuzi bila antenna.

"Azam tv imekuwa na nia madhubuti ya kiwafikia wananchi wote, mjini na vijijini, ndani na nje yanchi,na kuhakikisha tumejiimarisha kuwapa maudhui Bora, Bidhaaa Bora za kisasa kabisa, kwenye Huduma zetu zote Ili kusambaza  burudani Kwa wote Kwa Bei nafuu Zaidi" amesema Loth Mziray.
 






Nae Kwa upande wake Afisa Mauzo na usambazaji wa Azam Adam Ndimbo  amesema mwanzo tuliweza kufika mikoa 11 ikiwemo hivyo mikoa 6 iliyoongezeka inakamilisha idadi ya Mikoa 17 Kwa kupata burudani sio utani.

Previous Post Next Post