Baraza la ushauri la watumiaji wa Huduma za usafiri Ardhini (LATRA CCC) limeiomba serikali Kwa kutumia Sheria ya serikali za Mitaa na mipango ya mwaka 1982 kuweka utaratibu wa kufaa wa kuwa na vituo venye sifa Ili kuendana na mahitaji ya watumiaji na Haki ya Msingi ya Usalama wa abiria,Muda na gharama za safari.
Akizungumza na waandishi wa Habari Kaimu Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Leo Ngowi amsema baraza linatumbua uwekezaji mkubwa unafanywa na serikali kwenye miundombinu mbalimbali Nchini, ikiwemo kituo Cha mabasi ya Magufuli.
"Ni kweli kuwa wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na Abiria wanahitaji, vituo vikubwa vyenye miundombinu ya kutosha Kwa ajili ya Usalama wa kukidhi mahitaji mbalimbali ya Jamii hasa abiria kisafiri Kwa wakati, gharama nafuu ma Kwa usalama"amsema Leo Ngowi
Aidha amsema Baraza kupitia vyombo vya habari waliona mvutano mkali kati ya Abiria na wasimamizi WA Sheria juu ya kushukia stendi ya mabasi ya Magufuli iliyopo mbezi Luis jijini Dar es salaam.
Amsema Ili kuondoa mvutano kati ya Abiria na wasimamizi wa Sheria baraza linaomba serikali iendelee kuruhusu abairia kutumia Huduma zilizopo , wakati ikijipanga na kuweka utaratibu wa kumsaidia abairia Kupata Huduma Bora, Salama Kwa wakati na Kwa gharama nafuu.