KAMPUNI YA PARIMATCH YADHAMINI TIMU YA MBEYA CITY KATIKA MSIMU, 2022/2023.



Na Lilian Ekonga 

Kampuni ya Parimatch inayoendeaha shughuli za michezo ya kubashiri mtandao wameongia Rasmi makubaliano ya mkataba WA udhamini WA kablu ya Mbeya  City Ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara Katika Msimu wa  mwaka2022/2023.

Akizungumza na waandishi wa Afisa Habari wa Pari Match Isamil Mohammed amsema mbeya City ni Moja ya kablu kubwa  na idadi ya mashabiki na ushawishi Katika soka na hiyo ndio sababu tosha ya wao kurejea Tena kufanya udhamini na Mbeya City kwa msimu huu mpya.

Amsema Parimatch mkataba Huo utajumuisha na Utoaji vifaa kwa kablu Pamoja  ukarabati mdogo wa uwanja wasokoiene hasa Katika eneo la kukaa benchi la ufundi kwa awamu  Ili kufanya Uwanja  kuendelea kuwa na sifa ya kuchezewa michezo ya Ligi Kuu.



"Tunaendelea na michakato mbalimbali ya kuunga mkono vilabu Vingine kutoka ligu Kuu, Ligi daraja la kwanza  na hata vilabu chupukizi , ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na bodi ya Ligi kuhakikisha Ligi za Tanzania na tuanenda kimataifa"amsema Ismail Mohammed.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Mbeya City FC, Emmanuel Kimbe aliwaahidi Parimatch ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kile wanachotakiwa kukifanya Lakini pia aliushukuru uongozi wa Parimatch kwa kufanya kazi nao kwa msimu huu mwingine wa 2022/23.

"Kwetu mmekuja sehemu sahihi na hamtojutia kuwa na sisi hivyo tutawapa Kile mnachohitaji, " 

Pia Kimbe aliwashukuru Parimatch kwa kuwarekebishia uwanja wa sokoine ambao utasaidia Watu wote wanaotumia uwanja huo ambao utaongeza Uchumi wa jiji la Mbeya.


Previous Post Next Post