NAIBU WAZIRI KATAMBI AMEZITAKA TAASISI ZA KIRAI KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIJANA.



Na Lilian Ekonga

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi amezitaka asasi za kiraia nchini zinazojihusisha na vijana kujikita zaidi katika kutatua changamoto za vijana badala ya watendaji wa taasisi hizo kujinufaisha kupitia taasisi.

Hayo yamesemwa katika kongamano la vijana jijini Dar es Salaam ambapo Katambi amesema asilimia 60 ya taasisi hizo zimesajiliwa kujihusisha na vijana ambapo zimekuwa zikipokea fedha kutoka kwa wafadhili hivyo kuhakikisha zinaleta matokeo chanya kwa changamoto zinazowakumba vijana.



Aidha Naibu waziri Katambi amewaasa vijana walioaminiwa katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo katika sekta binafsi na taasisi za umma kufanya kazi kwa weledi ili kutoharibu taswira ya vijana kuaminiwa kushika nafasi mbalimbali.

Hata hivyo Katambi amesema katika kukabiliana na tatizo la ajira nchini serikali imeweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi ili kuwekeza ili kuhakikisha ustawi wa maisha ya Watanzania hasa kundi la vijana.

Kwa upande wa Baadhi ya vijana katika kongamano hilo wameeleza namna gani vijana wanaweza kutumia changamoto zinazowakumba kugeuza kuwa fursa ikiwemo fursa zinazopatikana katika kilimo.

Kongamano la vijana limeandaliwa na vijana wenyewe Kwa kushirikiana na mashirikaya vija tokea kafa mbali mbali mbali na wenye ubobevu Katika taaluma tofauti baada ya kuchambua na kusoma mahitaji ya vijana Katika  kiwango Cha kitaifa, kikanda na kimataifa.



Previous Post Next Post