DC JOKATE AHAMASISHA WANANCHI WA WILAYA YA TEMEKE KUJITOKEZA NA KUSHIRIKI KATIKA SIKU YA SENSA ITAKAYOFANYIKA TAREHE 23 MWEZI HUU.



Katika kuelekea siku ya sense na makazi ya watu itakayofanyika tarehe 23 mwezi huu, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo amewahamasisha  Wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza na kushiriki kwa wingi ili kuipatia fursa serikali kuweka mikakati muhimu katika Taifa.

Amesema hayo leo kwenye Bonaza kutwa lililofanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala vilivyopo katika wilaya hua Temeke na kuhudhuriwa na Viongozi Mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Naibu Meya na Madiwani wa wilaya hiyo na Baadhi ya Wasanii wa Bongo Fleva Juma Nature, Yamato Band na wengineo.



Amsema Siku hiyo ni ya mapumziko na  mahususi kutoa nafasi kwa Wananchi wote kuweza kushiriki bila kuwa na sabbabu zingine kwenye zoezi hili la sensa

“Nawaomba Wananchi wenzangu wa Temeke tume watulivu, tuonyeshe ushirikiano kwa Makarani watakaofika kwenye maeneo yetu” amesema DC Jokate





Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Elihuruma Mabelya amezidi kuwasisitizia  Wananchi wa wilaya hiyo kuwaitiske zoezi la Sensa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

“Zoezi la Sensa ni muhimu, hamasa imefanyika na leo ni hitimisho la hamasa ambayo Mkuu wetu wa Wilaya ameifanya Usiku na mchana. Wilaya yetu ina mitaa 142 na kata 23 ambayo inahitaji maendeleo” amesema Mabelya.

Tukumbuke siku ya Tarehe 23 mwezi huu wa nane mwaka 2022 itakuwa sensa ya makati na watu itakayofanyika Nchi nzima na siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko kitaifa.
Previous Post Next Post